Na Pamela Mollel,Arusha

Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)  itaanza kununua shehena ya mafuta moja kwa moja kutoka kwenye mitambo ya wazalishaji mafuta wazalishaji  badala ya kununua mafuta hayo kwa watu wa kati ili kubidhiti mfumuko wa bei hapa Nchini

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Arusha, Waziri wa Nishati, January Makamba alisema serikali iliiwezesha TPDC kushiriki zabuni ya kishindani na makampuni mengine ya kimataifa ambayo kila mwezi yanaleta mafuta nchini

Alisema TPDC imefanikiwa kushinda sehemu kubwa ya zabuni hiyo kwa kutoa bei ndogo zaidi ya kuagiza mafuta ya dizeli nchini kwa mwezi Desemba mwaka huu

Aliongeza kuwa katika kudhihirisha hatua hiyo kuwa ya manufaa mwezi Agosti 2021,wakati bei ya mafuta ghafi duniani ilikuwa dola 73 kwa pipa, kampuni iliyoshinda zabuni ya kuleta mafuta ya dizeli nchini iliuza kwa dola 30 kwa  tani za ujazo (premium).

" licha ya bei ya mafuta ghafi kupanda duniani na kufikia dola 86 kwa pipa,TPDC italeta dizeli nchini Desemba mwaka huu kwa wastani wa dola 20 kwa tani za ujazo"alisema Makamba

Alisema pia katika ziara yake aliyoifanya nchi zinazouza mafuta akiwa na watendaji wengine wamefanikiwa kushawishi Nchi rafiki kujenga kituo kikubwa cha upokeaji na uhifadhi mkubwa wa mafuta(fuel terminal) kwaajili ya soko la ndani ya nchi lakini kwa mahitaji ya nchi za Afrika Mashariki na Kati na nyinginezo za mbali pale itakapohitajika

Alisema endapo kutatokea dharura huko Duniani na kushindwa kuagiza mafuta kiasi cha mafuta yaliyopo nchini yanatosheleza kwa wastani wa siku 15 tu

Alisema katika hatua ya muda mfupi kuiimarisha TPDC kwakuruhusu haraka kuajiri watumishi weledi na wajuzi wa biashara wa biashara ya mafuta ili iendelee kununua mafuta kwaniaba ya serikali kwa ufanisi zaidi

Pia kupitia mfumo wa uagizaji wa mafuta wa pamoja(bulk Procurement Reserve)ili kubaini mapungufu na kuboresha kwa kiwango kikubwa ikiwemo kufanya tathimini ya utendaji na watumishi wa taasisi zote za serikali zinazohusika na biashara ya mafuta ikiwemo TPDC,EWURA na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta wa  Pamoja(PBPA) ili kuhakikisha kuwa taasisi hizo na watumishi wake wanatimiza wajibu wao kwa weledi

Alisema katika kuendelea na utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Hassan Suluhu ni kuendelea kupitia tozo na kodi mbalimbali zinazochangia kuongezeka kwa bei ya mafuta nchini pia serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kibiashara na sekta binafsi ili kuwe na ushindani wa haki na uwazi kwa !anufaa ya watumiaji mafuta nchini

Alisisitiza serikali itaongeza ufuatiliaji wa karibu zaidi kwenye sekta ya mafuta kwakutumia vyombo na mamlaka mbalimbali ili kubaini na kudhibiti hujuma na udanganyifu katika biashara ya mafuta ikiwemo uwekaji wa adhabu kali zaidi ikiwemo kunyang'anywa leseni pale itakabyobainija hivyo

Alisema pia serikali itaboresha miundombinu ya upokeaji na uhifadhi wa mafuta nchini hasa katika bandari ili kuhakikisha kunaufanisi zaidi ikiwemo kufanyia kazi mapemdekezo ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kuhusu biashara ya mafuta nchini

Hata hivyo Makamba alisisitiza kuwa bei ya mafuta nchini kwakiasi kikubw inachangiwa na  bei ya mafuta

Duniani ambazo serikali inanafasi ndogo kwenye kudhibiti hata hivyo serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha yaliyoko ndani ya uwezo wa serikali katika kudhibiti bei ya mafuta yanafanyiwa Kazi.

Waziri wa Nishati January Makamba akizungumza na waandishi (hawapo pichani) jijini Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...