*Wasema imekuwa mwiba wa maendeleo ya kidigitali Tanzania, waeleza sekta ya habari ilivyoathirika
Na Mwandishi Wetu
WADAU
wa sekta ya habari na hasa waliojikita katika kutoa huduma za maudhui
katika Tovuti, programu tumishi, mtandao wa YouTube na blogs
wamelalamika kupungua kwa kasi kwa watumiaji wa huduma zao huku
wakiiomba wizara na wadau husika kujadili na kulipatia mwarobaini suala
hili.
Kupungua kwa watumiaji hao kunatokana na kupanda maradufu
kwa bei za vifurushi vya interneti nchini, huku GB 1 ya Data ikipatikana
kwa zaidi ya dola 1.3 ambapo kumesababisha kupungua kwa kasi idadi ya
watumiaji wa internet nchini, hivyo kuathiri taasisi, mashirika na
watumiaji binafsi wa interneti ambao hutumia huduma hiyo katika majukumu
mbalimbali pamoja na burudani.
Taarifa iliyoandaliwa na
baadhi ya watoa maudhui, waandishi wa habari za mtandaoni na watumiaji
wa mitandao Tanzania wamesema kutokana na bei hizo kutokuwa rafiki kwa
watumiaji wa huduma hiyo hasa mwananchi wa kawaida Taasisi na tasnia
mbalimbali zimetajwa kuathirika kwa namna moja au nyingine.
Wamesema
kuwa ili kuendesha mitandao ya kijamii inatakiwa kutumia bando kila
wakati ili kuendelea kuuhabarisha umma kuhusu habari na matukio
mbalimbali hivyo gharama kubwa za vifurushi zimekuwa kikwazo kwa
bloggers & youtubers.
Kwa upande wa Wasanii na watoaji
maudhui ya burudani hasa kwa mtandao wa video wa YouTube nao wamedai
idadi ya wanaofuatilia kazi zao kushuka kwa kasi kwa siku za karibuni,
jambo ambalo wamedai kuathiri sana kipato chao. Vilevile mitandao
mbalimbali ya takwimu inaonesha kushuka kwa watumiaji wa mtandao wa
YouTube Tanzania kwa siku za karibuni.
Wakati kwa watumiaji
binafsi wa internet nchini Tanzania nao wameonesha kukerwa na kupanda
mara kwa mara kwa bei za vifurushi tena vinapandishwa kimya kimya licha
ya mamlaka kusema gharama zimeshuka huku wakidai uishaji wa haraka
kuliko kawaida wa vifurushi hivyo, vile vile wanakumbusha ahadi za
wadau na wizara kuahidi mara kadhaa kulishughulikia tatizo hilo na
kubakia ahadi hewa.
Pamoja na hayo, bei hizi ambazo zimetajwa
kutokuwa rafiki kwa watumiaji huenda zikazidi kuathiri mfumo mzima wa
maendeleo ya kidigitali hasa kwa mashirika, taasisi, na makampuni kama
vile huduma za kibenki za kidigitali, huduma za afya, elimu, na dini
zinazopatikana kwa njia za kidigitali pamoja na tasnia ya michezo ya
bahati nasibu ya mtandaoni.
Pamoja na hayo wamedai hali hiyo
imeathiri haki ya kupata taarifa huku wakifafanua kila mtu ana haki ya
kupata taarifa, kwa miaka ya karibuni kutokana na ukuaji wa maendeleo ya
teknolojia ya habari na mawasiliano hata Serikali imekuwa ikitoa
taarifa zake kwa idara mbalimbali kwenda kwa wananchi kwa njia ya
mitandao.
Hiyo inahusisha hata Matangazo ya moja kwa moja ya
Uapisho wa viongozi, uzinduzi wa miradi na hotuba za viongozi kwa
wananchi ambao wapo maeneo tofauti tofauti. Kwa mujibu wa wadau hao
wamesema hapo awali ilikuwa rahisi mtu kufatilia mubashara matangazo ya
matukio ya kitaifa kupitia mtandaoni.
Lakini hivi sasa wananchi
wengi wanapata shida kuangalia hadi mwisho matangazo hayo kwani
maranyingi kabla tukio halijaisha kifurushi cha data kinakuwa
kimeshaisha, hivyo athari hizi si tu kwetu wananchi ila hata kwa watoa
taarifa wakiwemo viongozi wa Serikali.
Na hivyo ujumbe uliokusudiwa kuwasilishwa kwetu wananchi unakuwa umekwamishwa na gharama za vifurushi vya data.
Kutokana
na hali hiyo wadau mbalimbali wanaishauri wizara husika, pamoja na
kampuni za simu nchini yanayotoa huduma hiyo muhimu kwa maendeleo
kuangalia upya na kwa umakini jambo hili kwa maendeleo na tija ya nchi.
Wamesema
wanafahamu Vifurushi vya Data ni Ofa za kampuni ya simu katika kufanya
ushindani wa kibiashara, lakini licha ya ofa basi wanashauri ziwe zenye
kuleta unafuu kwa mwananchi kwani kukiwa na huduma hizo nzuri, hata
matumizi ya mawasiliano kwa njia ya simu yataongezeka na kutaongeza
mapato kwa Serikali kwa njia ya kodi na tozo zilizopo hivi sasa.
Home
HABARI
WADAU WATOA OMBI KWA WIZARA,KAMPUNI ZA SIMU KUANGALIA NAMNA YA KUPUNGUZA BEI KUBWA KATIKA VIFURUSHI VYA DATA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...