Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeshiriki Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania kwasababu ni Maonesho yanayohusu Viwanda na Bidhaa zake, hivyo BRELA kwa majukumu yake kisheria inatumia fursa ya Maonesho hayo kuhamasisha wenye viwanda kusajili alama za biashara na huduma ili kulinda umiliki wa alama zao. Pia BRELA imelenga kuwahamasisha wafanyabiashara  kurasimisha biashara zao ili wajulikane katika Sekta


Bw Davide Firno mwekezaji nchini Tanzania akipata elimu na usaidizi wa sajili kutoka BRELA kwenye Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania  yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Zanzibar wakipata elimu ya namna BRELA inavyotekeleza majukumu yake walipotembelea banda la BRELA kwenye Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara

Bw Gaston Canuty akipata usaidizi wa karibu wa namna ya kufanya mabadiliko ya taarifa ya kampuni kutoka kwa Paul Peter Afisa kutoka Brela.  BRELA inashiriki Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania  yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara.




 Bw Issa Ally Njoka mzalishaji wa bidhaa ya Lishe akipata elimu ya Alama ya Biashara juu ya bidhaa anayozalisha kutoka kwa Bw Raphael Mtalima Afisa Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Haki Miliki. BRELA inashiriki Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania  yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...