NA BALTAZAR MASHAKA, Magu


MKUU wa Wilaya ya Magu,Salum Kalli amewaongoza wananchi wa wilaya hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan,kwa uamuzi wake wa busara wa kuruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kurejea shuleni kuendelea na masomo.

Walitoa pongezi hizo jana baada ya Mkuu huyo wa Nchi kutangaza kuwaruhusu wanafunzi waliokatiza masomo yao kwa kwasababu ya kupata mimba kurejea masomoni kwenye shule za msingi, sekondari na vyuo.

Taarifa za Shirika la Afya Duniani takribani wasichana 14 hadi 15 milioni hupata ujauzito katika umri mdogo, hali inayotumbukiza wasichana wengi katika wimbi la umasikini na kupoteza ndoto zao hasa za elimu.

Pia chagamoto ya mimba za utotoni imekuwakumba watoto wa kike wa kuanzia umri wa miaka 10 hadi 19 wanapopata ujauzito na kujifungua mbapo mara nyingi kundi la umri huo huwa shuleni katika ngazi ya msingi au sekondari.

Sababu za watoto wengi wa kike kupata ujauzito katika umri mdogo ni pamoja na ukosefu wa elimu hasa ya afya ya uzazi, umasikini,usawa wa kijinsia, ndoa za utotoni,ubakaji na ukatili wa kingono.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana kuhusu uamuzi huo wa Rais Samia,Mkuu huyo wa Wilaya na baadhi ya wananchi walisema ni hatua kubwa ya muhimu itakayosaidia watoto wa kike kutimiza ndoto walizojiwekea maishani.

Walisema hatua hiyo ni kubwa kwa serikali,jamii na kwa wasichana ambao kwa miaka mingi walikosa haki ya kupata elimu kwa sababu ya kupata ujauzito shuleni, pia kukosekana kwa mfumo rasmi wa kurudi shule kuendelea na masomo.

Kalli,alisema Rais Samia kuruhusu wanafunzi waliokatishwa masomo sababu ya kupata ujauzito ni uamuzi wa busara unaopaswa kuungwa mkono ili watoto hao wapate fursa ya kuendelea na shule baada ya kukatishwa masomo ili watimize zao ni maono sahihi vijana walikosa haki ya msingi hasa mabinti.

Alisema watoto wa kike walitaka wafikie ndoto zao walizojiwekea maishani lakini wakakatishwa masomo na wanaume wakware si kwa kupenda, wengine wamesababishiwa,hivyo kuwarejesha waendelee na masomo ni jambo la kumshukuru Rais,baadhi wa maana wengine .

“Mheshimiwa Rais Samia,ni hakimu wa kweli,ameona tatizo hili kubwa na tunamshukuru sana kwa kuwanusuru watoto wa kike wasikae nyumbani, tumepambana na tumehangaika sana na hili la kesi za mimba kwa wanafunzi,ushahidi ulivurugwa na watuhumiwa wakishirikiana na baadhi ya wazazi kwa kupeana fedha na mali na hakuna kesi tulishinda,”alisema.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa elimu ni mtaji kwa mtu yeyote akisoma itampa faida maishani licha ya ruhusa hiyo, serikali haitasita kumchukulia hatua mtu atakayempa mwanafunzi ujauzito,inataka mtoto wa mkulima masikini apate haki ya elimu,tutendelea kuiunga mkono watoto wa kike wapate elimu kwa wakati bila vikwazo.

Alifafanua kuwa serikli imewapunguzi mzigo wananchi baada ya kutoa sh. bilioni 2.46 kujenga madars 123, hivyo uamuzi wa kuwarejesha shuleni waliopata ujauzito ni sahihi ili wayatumie wasome kwa uhuru na msimamo wa serikali kwa watakaobainika kuwapa mimba wanafunzi sheria ipo haijenda likizo.

Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Magu, Nyeoja Mkangar, alimshukuru Rais Samia, kutoa fursa kwa watoto wa kike walipata mimba wakiwa shuleni,wazazi wautumie uamuzi huo kama fursa ya kuwaendeleza badala ya kubweteka, wawabane wasijihusishe na vitendo vya ngono.

“Tusitumie fursa hiyo vibaya,watoto wafundishwe afya ya uzazi kuepuka mimba, serikali isifumbie macho tatizo la mimba,sheria iwabane wote (msichana na mvulana) kani kila mmoja ana fursa ya kuendelea na masomo,baada ya rais kutoa fursa hiyo kujitunza na kujifunza,”alisema.

Kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Magu na Katibu wa Vijana wilayani humo, Edward Mamba, alisema maono ya Rais Samia ni sahihi katika kutekeleza ilani ya uchaguzi kwenye sekta ya elimu kwani vijana hasa mabinti walikuwa wakikosa haki ya msingi ya kupata elimu sababu ya mimba,msichana akiwa na elimu maisha yake yataboreka kiuchumi na kijamii.

Aidha mkazi wa Kisesa, Tumikieli Ayo, alisema uamuzi huo ni mzuri ingawa una positive na negative (hasi na chanya) kwamba baadhi wanaweza kuutumia vibaya kama fursa kuwa hata mwanafunzi akipewa mimba atarejeshwa shuleni,pia msichana atakayerudi shuleni atakuwa akifikiria mwanaye zaidi kuliko masomo.

Naye Irene Ezekiel pia mkazi Kisesa, alisema anampongeza Rais Samia kuwarejesha shuleni watoto wa kike waliopata ujauzito baada ya kujifungua kutawawezesha kujiendeleza na kutimiza ndoto zao za maisha.

Jenifer Benjamin yeye alisema si wanafunzi wote waliopata mimba kwa kupenda la hasha, wapo waliobakwa na hali ya umasikini, hivyo kuwajeresha shuleni ni jambo zuri n kupita hao tunaweza kupata viongozi na wataalamu wa kesho.

Pia Amani Kisoka, alisema busara za Rais Samia zisipuuzwe ka sababu amesaidia kundi hilo la waathirika wa ujauzito kufufua matumaini ya kukamilisha ndoto walizojiwekea kupitia elimu badala ya kukaa nyumbani kulea watoto hata watoto wa kiume wanastahili kupata elimu maana kila mmoja ana ndoto alizojiwekea.

Ofisa Elimu Sekondari wilayani Magu,James Malima, alisema uamuzi wa Rais Samia kuwarejesha shuleni watoto waliopata mimba na kukatishwa ndoto zao, utakuwa na afya ambapo watwajengea uwezo wafikie malengo yao na kuchukua tahadhari.

Alisema wilaya hiyo ilipokea sh.bilioni 2.46 za kujenga vyumba 123 vya madarasa ili kukabiliana na uhaba wa miundombinu hiyo, vitakapokamilika changamoto hiyo itakwisha na hakuna mtoto atakosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwakani.
-Mkuu wa Wilaya ya Magua, Salum Kalli, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kuwarejesha shuleni kuendelea na masomo  wanafunzi waliopata ujauzito.
.Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Magu abaye nia ni Ktibu wa UVCCM wilayani humo, Edward Mamba, akitoa maoni yake baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuamua kuwarejesha shuleni wanafunzi wa kike waliopat ujauzito ili waendelee na masomo.Picha na Baltazar Mashaka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...