Taarifa zaidi msiba wa Rashid Zahor

Mhariri Msanifu Mkuu wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Rashid Zahor, amefariki dunia nyumbani kwa Dada yake Chanika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili, Dada wa marehemu, Asha Zahor, alisema kaka yake amefariki dunia saa tatu asubuhi baada ya kusumbuliwa na maradhi mbalimbali.

Alisema kabla ya umauti, marehemu Zahor alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari na shinikizo la damu kwa muda mrefu.

“Amefariki akiwa anaendelea na matibabu,  tulitoka hospitali baada ya  kusumbuliwa kwa maradhi muda mrefu, tukarudi nyumbani ilipofika saa tatu asubuhi alifariki,” alisema kwa majonzi.

Dada huyo wa marehemu alieleza kuwa, msiba  upo Chanika nyumbani  na maziko yatafanyika katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam saa 10.00 alasiri.

Alieleza kuwa, Zahor alikuwa ni mtoto wa pili na baada ya mtoto wa kwanza kufariki ndio alikuwa mkubwa wa familia yao yenye watoto tisa kwa Baba na mama mmoja.

Aliongeza kuwa baba wa Zahor  alishafariki dunia na walibaki na mama mzazi, hivyo Zahor amefariki akiwa amemwacha mama yake mzazi na nduguze saba.

Zahor alianza kwa kuandika hadithi katika magazeti ya Uhuru, akiwa mwandishi wa kujitegemea mnamo mwaka   1995 aliajiriwa rasmi na kuanza kuitumikia taasisi hiyo.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...