Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Njia ya Kilungule inayounganisha Kata hiyo na eneo la Buza Kwa Mpalange imeendelea kumomonyoka na kuwapa shida wapita njia, Madereva wa Magari na Bajaji katika maeneo hayo.

Usafiri wa Bajaji unaochukua abiria kutoka Buza Kwa Mama Kibonge hadi Kilungule zimelazimika kuishia kwenye eneo linapojengwa Daraja hilo (eneo maarufu Kwa Mpalange), huku Abiria hao wakilazimika kuishia eneo hilo kutokana na Bajaji hizo kushindwa kupita kwa sababu ya ujenzi wa Daraja unaoendelea.

Hata hivyo changamoto hiyo ya muda inaendelea kutatuliwa na Kampuni ya Group six international [G S I ] inayojenga Daraja litakalounganisha maeneo hayo bila changamoto yoyote kwa Watumiaji, huku mmoja wa Wasimamizi wa mradi wa ujenzi huo akitoa taarifa ya ujenzi kukamilika Januari 2022.


Baadhi ya abiria wamelazimika kutumia njia mbadala (yenye kifusi mbele) ili kuendelea na safari zao wanapotoka Kilungule kuelekea Buza Kwa Mpalange.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...