Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala wametakiwa kujisajili, kuorodhesha wasaidizi wao, kusajili vituo, pamoja na dawa wanazotumia kutibu wagonjwa. 

Agizo hilo limetolewa leo na Mwenyekiti-Baraza la Tiba Asili/Mbadala Prof. Hamis Malebo alipokuwa anaongea na waandishi wa habari Jijini Dodoma.

Prof. Malebo amesema kuendelea kufanya matibabu bila kupata kibali kutoka katika Baraza la tiba asili na tiba mbadala ni kosa kisheria.

Amesema waganga wote ambao hawajajisajili wanatakiwa wawe wamejisajili kabla tarehe 31 machi, 2022 na baada ya hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale watakaokiuka agizo hili.

“Nawataka waganga wote kujiepusha na vitendo vyote vinavyokinzana na Sheria, kanuni na taratibu zilizopo, ikiwa ni pamoja na kacha kuweka mabango yanayopotosha jamii, kurusha matangazo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii bila ya kuwa na Kibali kutoka Baraza.” Amesema Prof. Malebo

Aidha, amewataka wanaouza Dawa kiholela kwenye vyombo vya usafiri, nyumba za ibada, sokoni na sehemu zenye mikusanyiko, kuacha tabia hiyo kwakuwa Dawa zote za Asili zitauzwa katika maduka ya Dawa yaliyosajiliwa.

Hata hivyo Prof. Malebo amewataka wanaotoa elimu na kutangaza huduma zinazohusisha Tiba Asili na Mbadala kwenye Vituo vya redio na runinga nao kupata kibali kutoka Baraza.

Kwa upande wake Msajili-Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Dkt. Ruth Suza amewataka waganga kuwa makini katika utoaji wao wa huduma sababu wanahusika moja kwa moja na Afya za wananchi.

Hivyo, Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kupitia Mwenyekiti Prof. Malebo limepiga marufuku kuanzia leo kuacha kurusha Matangazo yote ambayo hayajapitishwa na Baraza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...