Na Mwandishi wetu, Simanjiro
ASKOFU wa Good News For All Ministry, Dkt Charles Gadi amewaongoza wachungaji wa madhehebu mbalimbali kwa ajili ya maombi maalum ya kumuomba Mungu ili mvua inyeshe Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara na kuondoa ukame.

Maombi hayo yamefanyika baada ya kutokea ukame Wilayani Simanjiro na kusababisha mifugo 62,583 kufa Kwa kukosa maji na malisho.

Askofu Dkt Gadi ameongoza maombi hayo na kushirikisha wachungaji wa madhehebu tofauti wa mji mdogo wa Mirerani.

Amesema wameandaa maombi hayo baada ya kusoma kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa ukame umesababisha mifugo mingi kufa Simanjiro.

"Mifugo 62,583 kufa kwa ukame siyo jambo dogo hivyo tumemuomba Mungu ili inyeshe mvua isiyo na madhara kwa jamii na isiharibu miundombinu," amesema Askofu Dkt Gadi.

Amesema walianza maombi ya mvua tangu mwaka 2006 kwenye eneo la jangwani jijini Dar es salaam na wakazunguka mikoa mbalimbali ili kuomba mvua na kutokomeza ukame.

"Kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alishatoa wito kwa watu wa dini zote kumuomba Mungu nasi tumeungana madhehebu tofauti kuombea mvua," amesema Askofu Dkt Gadi.

Mchungaji wa Good News For All Ministry, Bezaleli Masawe amesema kusudi la kuomba mvua limedhamiriwa na viongozi hao wa dini kwa lengo la kuondoa ukame kwenye eneo hilo la Simanjiro.

Mchungaji Massawe amesema pamoja na kuomba mvua jamii inao wajibu wa kutunza mazingira, vyanzo vya maji na misitu ya asili.


"Tunatoa wito kwa serikali, mashirika na watu binafsi kuhakikisha vyanzo hivyo vinalindwa ili kusaidia hali endelevu ya utunzaji mazingira," amesema mchungaji Massawe.


Mchungaji Saimon Kefa wa kanisa la Moria Pentekoste amesema katika maombi hayo pia wamemuombea Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wa serikali wawe na afya njema.


Mchungaji Kefa amesema wameomba mvua inyeshe, wamewaombea viongozi wa kitaifa, wameombea uchumi kwa watu na amani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...