Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na viongozi na wataalamu wa mazingira alipotembelea chanzo cha maji cha Usa River mkoani Arusha Januari 18, 2022.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo Waziri Jafo akipanda mti na wanafunzi wa shule ya sekondari Midawe iliyopo wilaya ya Arusha wakati wa ziara ya kukagua shughuli za mazingita mkoni Arusha Januari 18, 2022.


Na Robert Hokororo, Arusha

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo Waziri Jafo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuvitunza vyanzo vya maji vilivyopo nchini ili kwa kupanda miti.

Ametoa wito huo Januari 18, 2022 alipofanya ziara ya kikazi mkoani Arusha ya kukagua vyanzo vya maji na vitalu vya miti katika Halmashauri ya Meru pamoja na kuhamasisha wananchi kushiriki kampeni ya upandaji miti.

Dkt. Jafo alipongeza jitihada za uongozi wa Halmashauri za Arumeru na Arusha katika kusimamia vizuri vyanzo vya maji vya Usa -River na Midawe pamoja na kuendelea kuhamasisha wananchi kupanda miti.

Alisema kuwa hivi sasa hali ya mabadiliko ya tabianchi imeshamiri kiasi cha kuleta madhara ya kimazingira hivyo kila mmoja anawajibika kushiriki kikamilifu katika kulinda vyanzo vya maji.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa utunzaji wa mazingira Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelekeza utunzaji wa mazingira kuwa ni agenda ya kudumu.

“Ndugu zangu hatuna mbadala wa Suala la utunzaji wa mazingira, tumeanza kushuhudia athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, hapa Arusha tunaona kiwango cha joto kimeongezeka na ha ta mikoa mingine niwasihi tutunze vyanzo hivi vya maji,” alisisitiza Waziri Jafo.

Pia alisisitiza umuhimu wa kila mwananfunzi kupanda mti na kuutunza ili kutimiza lengo la kua na miti ya kutosha ambayo ni suluhisho la athari za mabadiliko ya tabianchi.

Katika ziara hiyo pia alifanya ziara katika shule ya sekondari Midawe iliyopo halmashauri ya Arusha ambapo alishiriki katika zoezi la kupanda miti ikiwa ni sehemu ya kampeni ya upandaji miti.

Kwa upande waqke Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango alimshukuru Waziri Jafo kwa kufanya ziara wilayani humo na kukagua hali ya utunzaji wa mazingira.

Mhandisi Ruyango aliahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na kuwa atahakikisha kila mwanafunzi anapanda mti mmoja pamoja na kuwa na bajeti ya kutosha kwa ajili ya shughuli za mazingira katika halmashauri zote mbili za Wilaya ya Arusha.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...