Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAOFISA 13 na askari 27 wa Jeshi la Uhifadhi la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) wameanza mafunzo ya elimu ya usalama baharini,ikiwa ni sehemu ya Wakala huo kuwajengea uwezo watumishi wake kutekeleza majukumu yao hasa ulinzi wa mikoko baharini.

Mafunzo hayo yameanza rasmi Januari 12 na yanatarajia kumalizika Januari 25 mwaka huu ambapo maofisa na askari hao watapatiwa mafunzo hayo sambamba na kupewa mbinu mbalimbali za kukabiliana na watu wote wenye kuvamia na kuharibu mikoko iliyopo Pwani ya bahari.

Akizungumzia kwa niaba ya Kamishna wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Profesa Dos Santos Silayo, Kamishna Uhifadhi Msaidizi TFS Kanda ya Mashariki Caroline Malundo amesema mafunzo hayo ni muhimu katika utekelezaji wa majukumu yao ndani ya taasisi na nje ya taasisi inapobidi.

"Kama tunavyofahamu kwa sasa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imekuwa Jeshi kamili na umeweka kipaumbele katika kuboresha mazingira ya utendaji kazi maeneo ya bahari ikiwemo ununuzi wa boti,vifaa vya kujiokolea maofisa na askari wanapokuwa Katika kutekeleza majukumu yao baharini kama vile koti za kujiokolea .

"Pia kuboresha na kuimarisha mifumo mbalimbali ya mawasiliano baharini,utoaji wa mafunzo ya usalama binafsi wakati utekelezaji wa shughuli za mikoko,uokoaji wa binadamu ikitokea dharura wakati wa doria za baharini .Lengo ni kuhakikisha mikoko na rasilimali nyingine za bahari zinalindwa ipasavyo.

"Mafanikio ya TFS kwa jeshi kamili wote tumeyaona na tumeshuhudia shughuli za uhifadhi wa mikoko zilivyoboreshwa na uhifadhi ulivyozidi kuimarika siku hadi siku.Hivyo kupitia mafunzo haya ni muhimu sana kwa watumishi wa TFS katika kuimarisha utendaji kazi wetu,lazima tuwe tayari kwa mapambano na mafunzo haya ya usalama baharini yanakwenda kutuimarisha,"amesema Malundo.

Akifafanua zaidi kuhusu mafunzo hayo, Kamanda Malundo amesema askari na maofisa hao wanatoka katika Kanda za mikoko za Mashariki (Dar es Salaam na Pwani), mikoa ya Kusini( Lindi na Mtwara) na Kaskazini (Tanga)."Niwaombe wote mnaoshiriki mafunzo haya mzingatie na kuelewa mafunzo haya

"Ambayo yatakuwa na msaada mkubwa sana katika kutekeleza shughuli zenu za ikiwa Uhifadhi upande wa mwambao mwa bahari,hususani kuzuia uhalifu na uharibifu wa rasilimali za mikoko."

Aidha amesema mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni utekelezaji wa mpango mkakati wa TFS wa mwaka 2020/2025 wa kuwajengea uwezo watumishi wa Wakala huo wanaofanya katika mazingira ya Pwani ya bahari. Na mwaka 2021/2022 tunatoa mafunzo haya kwa maofisa 13 na askari 27 ambayo ndio yamefunguliwa.

Kuhusu uharibifu wa mikoko na rasilimali zilizopo Pwani ya bahari,Kamanda Malundo amesema kutokana na hatua mbalimbali ambazo TFS imezichukua chini ya Profesa Silayo wamefanikiwa kudhibiti uharibifu wa mikoko ukilinganishwa na siku za nyuma.

Hivyo amesisitiza Wakala huo utaendelea kutoa mafunzo hayo kwa watumishi kadri inavyowezekana ili kuhakikisha rasilimali za mikoko zinalindwa ipasavyo bila kuwa na kisingizio chochote.

Awali Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti wa Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) EIleen Stanford Nkondola akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa FETA Dk.Semvua Mzighani amesema wao wapo tayari kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wa TFS.

Kamishna Uhifadhi Msaidizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Mashariki Kamanda Caroline Malundo ( kushoto) akitoa salamu ya kijeshi kwa maofisa na askari wa Jeshi la Uhifadhi wa Wakala huo ambao wameanza mafunzo ya elimu ya usalama baharini ikiwa ni mkakati wa kuwajengea uwezo wa kukabiliana na wahalifu wa rasilimali za mikoko ukanda wa Bahari.Kamand Malundo alikuwa amemwakilisha Kamishna wa TFS Profesa Dos Santos Silayo aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi
Maofisa na askari wa Jeshi la Uhifadhi la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) wakiwa katika ukakavu wakati Kamishna Uhifadhi Msaidizi wa TFS Kanda ya Mashariki Caroline Malundo akikagua gwaride aliloandaliwa kabla ya kufungua mafunzo ya elimu ya usalama baharini yaliyoandaliwa kwa watumishi hao .
Maofisa na askari wa Jeshi la Uhifadhi la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakiwa makini kumsikiliza Kamishna Uhifadhi Msaidizi wa TFS Kamanda ya Mashariki Caroline Malundo ( hayuko) pichani wakati akifungua mafunzo hayo
Kamishna Uhifadhi Msaidizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Caroline Malundo ( wa pili kulia) akipata ufafanuzi kutoka kwa Mkufunzi wa mafunzo hayo( wa kwanza kulia) kuhusu sensa za vidole    zinavyofanya kazi katika mwili wa binadamu.Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi( FETA EIleen Nkondola na wa kwanza kushoto ni mmoja wa maofisa wa  Ofisi wa jeshi hilo la Uhifadhi.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) EIleen Nkondola (kushoto) akiwa na Kamishna Uhifadhi Msaidizi wa TFS Kanda ya Mashariki Caroline Malundo ( kulia) wakati wa wakielekea kwenye ukumbi kwa ajili ya kufungua rasmi mafunzo ya elimu ya usalama baharini
Baadhi ya askari wa Jeshi la Uhifadhi la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) wakiwa makini kumsikiliza mmoja ya wakufunzo wa mafunzo hayo alipokuwa akitoa somo la uokoaji wakati yanapotokea majanga au ajali
Mkufunzi wa mafunzo hayo akitoa maelezo kwa maofisa na askari wa Jeshi la Uhifadhi TFS namna ya kumlaza mtu ambaye amepata majereha ili kumsaidia kunusuru maisha yake
Kamishna Uhifadhi Msaidizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Kanda ya Mashariki akisoma hotuba  wakati akifungua rasmi Mafunzo ya elimu ya usalama baharini kwa askari na maofisa wa Wakala huo
Baadhi ya maofisa wa TFS wakifuatilia mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakifanyika kwa askari na maofisa wa Jeshi la Uhifadhi la Wakala huo
Watumishi wa TFS wakifuatilia somo la uogeleaji baharini kwa vitendo wakati maofisa na askari wa Wakala huo waliopo kwenye mafunzo wakiendelea kuogelea kwa kuzama kwenye baharini
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...