Naibu  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete akiangalia moja ya nyumba iliyoathirika na mvua katika kijiji cha Makombe, Chalinze mkoani Pwani alipokwenda kutoa pole na kujionea athari za mvua

Naibu  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete akiwa ndani ya moja ya nyumba iliyoathirika na mvua katika kijiji cha Makombe, Chalinze mkoani Pwani alipokwenda kutoa pole na kujionea athari za mvua 

Naibu  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete akimsikiliza mmoja wa waathirika wa maafa ya mvua (aliyevaa kilemba) katika kijiji cha Makombe, Chalinze mkoani Pwani alipokwenda kutoa pole na kujionea athari za mvua 

Naibu  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete akizungumza katika moja ya nyumba iliyoathirika na mvua katika kijiji cha Makombe mkoani Pwani alipokwenda kutoa pole na kujionea athari za mvua

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete akielekea katika moja ya nyumba iliyoathirika na mvua katika kijiji cha Makombe, Chalinze mkoani Pwani alipokwenda kutoa pole na kujionea athari za mvua

……………………………………………..

Na Munir Shemweta, WANMM CHALINZE

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete ametembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika na mvua iliyoambatana na upepo kwenye jimbo la Chalinze mkoani Pwani na kutoa pole kwa wote walioathirika na mvua hizo.

Usiku wa kuamkia tarehe 20 Januari 2022 ilinyesha mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kwenye maeneo mbalimbali ya mikoa ya Pwani na Dar es Salaam ambapo katika jimbo la Chalinze mkoa Pwani takriban nyumba 36 zikiwemo shule mbili za msingi za Makombe na Bwilingu ziliathirika.

Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Jumamosi Januari 22, 2022 alitembelea familia za waathirika pamoja na shule mbili za msingi ambazo paa yake yaliezuliwa na mvua hizo.

Akiwa katika kijiji cha Makombe kilichopo kata ya Lugoba, Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwani alijionea athari iliyosababishwa na mvua hizo  ambapo aliwafariji waathirika na kuwaeleza kuwa, yeye kama mbunge kwa kushirikiana na halmashauri ya Chalinze wataangalia namna ya kuwasadia wale walioathirika na kadhia hiyo  ili waweze kurudi katika maisha yao ya kawaida.

“Binafsi yangu nieleze nimesikitishwa na janga lililotokea lakini wakati mwingine tuamini kila jambo limepangwa na Mwenyezi Mungu na lina sababu zake nyingi” alisema Ridhiwani.

Akiekezea uharibifu uliotokea kwenye shule ya Msingi Makombe, Ridhiwani ameagiza kufanyika jitihada za haraka ili kuyarejesha madarasa yaliyoathirika kurudi katika hali yake ya kawaida ili wanafunzi waweze kuyatumia kwa kuwa tayari shule zimefunguliwa.

“Binafasi namshukuru Mungu kwa sababu katika taarifa yenu hatukupata taarifa ya mtu aliyeumizwa kwa sababu wakati mwingine inapotokea wanafunzi wako darasani  inakuwa ni hatari sana na kushukuru chama kwa kutoa kipaumbele kwa maisha ya watu” alisema Ridhiwani. 

Katika kinachoonekana kuunga mkono hatua zinazofanyika kutokana na kadhia iliyotokea kwa madarasa ya shule, Mbunge huyo wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani alitoa kiasi cha shilingi milioni 5 ili kusaidia kurekebisha sehemu zilizopata athari ya mvua ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Possi  alimueleza Naibu Waziri Ridhiwani kuwa, mvua iliyonesha mbali na kuezua mapaa ya takriban nyumba 36  lakini mvua hiyo pia ilileta athari kwa shule mbili za msingi za Makombe na Bwilingu A.

Hata hivyo, alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo, ofisi yake ilianza kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kufanya tathmini ya uharibifu uliotolea shule ya msingi Makombe na kuahidi ndani ya wiki moja madarasa kuanza kutumika.

“Kule katika kijiji cja Makombe tatizo ni kubwa zaidi ambapo hatua tumeanza kuchukua kama halmashauri na leo mbunge ametuongezea nguvu, katika gharama ya milioni 26 anatuongezea milioni 5 na hela ikiingia itasaidia zaidi” alisema Possi.

Kwa upande wake Diwani wa Bwilingu Nasser Karama alieleza kuwa, mvua iliyonesha imeleta athari kwa baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Bwilingu pamoja na shule ya msingi Bwilingu ‘A’ ambapo baadhi ya wananchi wamepata hifadhi na kusaidiwa vyakula na wadau mbalimbali.

Hata hivyo, alikishukuru Chama cha Mapinduzi pamoja na Mbunge wa jimbo la Chalinze kwa kuchukua hatua za haraka mara baada ya kupata taarifa ya kutokea kwa maafa hayo ambapo alisema hatua hiyo imewafariji sana.

“Mie katika kata yangu nimeathirika hili darasa moja na nyumba ya mwalimu pamoja na madarasa yaliyochakaa ila tumepata tumaini baada ya kutembelewa na mbunge na mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze” alisema Karama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...