Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wakazi wa kitongoji cha Kisajanilo wamesema wako tayari kishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama hususani idara ya uhamiaji kudhibiti wahamiaji haramu wanaotumia njia ya Kijiji hicho kwenda nchi jirani ya Malawi

Wamesema hayo katika mkutano wa hadhara uliyoitishwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Njombe ukiwa na lengo la kushukuru kazi kubwa iliyofanywa na wanakijiji ya kukamata wahamiaji haramu 18 na mtanzania mmoja aliyekuwa amehusika kuwavusha

Katika mkutano huo kamanda wa uhamiaji mkoa wa Njombe kamishina mwandamizi msaidizi John Yindi amesema jukumu la kulinda nchi si la vyombo vya dola pekee bali ni pamoja na wananchi hivyo kitendo kilichofanywa na watu hao ni cha kuigwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...