Bodi ya Wakurugenzi ya PSPTB chini ya mwenyekiti wake Jacob Kibona imeidhinisha matokeo ya watahiniwa 2,108 waliofanya mitihani ya 20, 21 na 22 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB).

Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi amesema kwa upande wa mitihani ya 20 ambayo ilifanyika kwenye mwezi wa Agusti mwaka 2020 watainiwa waliofanya mtihani hiyo walikuwa ni 1060 ambapo watahiniwa waliofaulu  ni 479 ambao watakuwa na mitihani ya marudio  ni 519  na waliofeli kabisa ambao wanatakiwa kurudia mitihani  yote ni watahiniwa 62.

Pia alisema kwenye mitihani ya 21 iliyofanyika Mwezi Novemba mwaka 2020 watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa ni 571 ambapo watahiniwa waliofaulu 216 ambao watakuwa na mitihani ya marudio  ni 321  na waliofeli kabisa ambao wanatakiwa kurudia mitihani yote ni watahiniwa 34

Amesema mitihani ya 22 iliyofanyika mwezi Juni mwaka 2021 watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa ni 477 ambapo watahiniwa waliofaulu 165 ambao watakuwa na mitihani ya marudio  ni 262  na waliofeli kabisa ambao wanatakiwa kurudia mitihani yote ni watahiniwa 50.

“Jumla ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo walikuwa ni 2,108 ambapo watahiniwa 860 wamefaulu mitihani ya Bodi hiyo, watahiniwa 1,102 wamefeli somo moja au zaidi ambapo watakiwa kufanya marudio ya mitihani hiyo na waliofeli jumla yake ni 146 na hao wanatakiwa kurudia mitihani yote ya Bodi.” Alisema Mbanyi

Taarifa za matokeo haya zinapatikana kwenye tovuti ya Bodi hiyo ambayo ni www.psptb.go.tz ambapo mtahiniwa  anaweza kuona matokeo yake kupitia akaunti yake.

Pia dirisha la usajili kwa ajili ya mitihani ya Mei, 2022 linafunguliwa kuanzia terehe 24/01/2021

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa anatangaza matokeo ya mitihani ya Bodi ya 20,21 na 22 yaliyoidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi wa PSPTB makao makuu ya Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...