Na John Mapepele- WUSM

Naibu Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Said Yakub, amesema Tamasha la Utamaduni la makabila ya Mkoa wa Kilimanjaro linalotarajiwa kufanyika Januari 22, 2022 litafungua milango ya utalii wa kiutamaduni na kuvuta wageni mbalimbali kutoka duniani kote.

Akizungumza wakati alipokuwa akikagua maandalizi ya tamasha hilo kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi, leo Januari 19, 2022 mjini Moshi amesema maandalizi yanaendelea vizuri ambapo amefafanua kwamba tamasha hilo litajumuisha sanaa mbalimbali za makabila ya Wachaga, Wapare na Wamasai.

“Tunafurahi kuona tamasha hili ni mahususi kwa ajili ya kuenzi utamaduni lakini  kubwa zaidi litakuwa  ni fursa  ya  utalii wa kiutamaduni kwani  vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na  vyakula vya kiasili, vikundi vya nyimbo, mavazi na  michezo  mbalimbali  vitaonyeshwa  siku hiyo”. Ameongeza Yakub.

Aidha, amesema Wizara inatarajia kuendelea kushirikiana na wadau katika mikoa yote kufanya matamasha kama hili ili kukuza na kuendeleza  utamaduni wa makabila  mbalimbali, kukuza utalii wa kiutamaduni  na hatimaye kuongeza ajira  na vipato.

“Msingi wa taifa lolote ni utamaduni wake, Taifa lisilo na utamaduni ni taifa lililokufa, sisi kama Wizara tutaendelea kukuza na kuuenzi utamaduni wetu kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye”. Amesisitiza Yakub

Ametoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kushiriki kwenye tamasha hilo ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi.

Waziri mwenye thamana ya utamaduni nchini, Mhe. Mohammed Mchengerwa mara baada ya kuteuliwa  hivi karibuni kuiongoza  Wizara hiyo amesisitiza kuwa  karibu na wadau mbalimbali wa sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo kuanzia  katika ngazi za mtaa hadi taifa  ili kuleta mageuzi  makubwa kwenye sekta hizo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...