Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria umetia fora katika maonesho ya utamaduni wa chakula, bidhaa na vivutio vya utalii yaliyofanyika mnamo Januari 21, 2022 jijini Abuja.


Maonesho hayo, yaliyoratibiwa na Chuo cha Ulinzi cha Nigeria (Nigeria National Defense College - NDC) yalihusisha pia Balozi za nchi nyingine zaidi ya kumi zikiwemo Congo DRC, Cameroon, Cote D'Ivoire, Gabon, India, Nepal, Chad, Sierra Leone, Benin, Rwanda na Bangladesh. 

 

Kupitia maonesho hayo, Ubalozi uliweza kutangaza vyema bidhaa lukuki za Tanzania ikiwemo mvinyo, mazao ya mkonge, korosho, viungo, bidhaa za Ngozi za Wanyama, kahawa, majani ya chai na kadhalika. 


Vile vile ubalozi wetu ulionesha utamaduni wa Tanzania hususan chakula cha Kitanzania ikiwa ni pamoja na ugali, pilau na mboga za aina mbalimbali zilizovutia sana watu waliohudhuria.   


Vivutio vya utalii vya Tanzania kama vile mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro, Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na fukwe za bahari na mazao yake navyo vilinogesha uzuri wa banda la Tanzania ambalo lilisifiwa kwa ubora na wingi wa bidhaa.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...