Wenye ulemavu Njombe DC wabembelezwa kuchukua mikopo ya halmashauri.

Na Amiri Kilagalila,Njombe.
WATU wenye ulemavu halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani Njombe wametakiwa kujitokeza kuomba mikopo katika halmashauri ili kujikwamua kiuchumi.

Ombi hilo limetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli,wakati wa kukabidhi mkopo wa shilingi milioni 260 kwa vikundi 30,mkopo ukiwa na mchanganuo wa mashine na pikipiki na fedha ambapo alisema wenye ulemavu popote walipo wajitokeze kukopa mikopo ili kuwasaidia kiuchumi.

"Kwa hatua tulizofikia sasa kwa wale wenye ulemavu wanaoweza kufanya shughuli mbalimbali ujasiriamali ambao walikua wanakosa mitaji hakuna sababu sasa ya kuchukua bakuri kukaa barabarani na kuombaomba kwa sababu mama yetu Rais wa jamuhuri ya muungano Tanzania ameshatengeneza mazingira mazuri kabisa ya kuwawezesha na ndugu zetu wenye ulemavu"alisema Hongoli

Alisema kuwa"Niwaombe sasa badala ya kuchukua bakuri na kuombaomba kutembea misikitini kuombaomba kila ijumaa, basi tutumie fursa hii sasa ya mikopo ya wenye ulemavu tukope tupate mitaji tuweze kuendeleza shughuli zetu.Nimesema wenye ulemavu ambao wanaweza wengine wanaoweza kufuga hata kuku wakafuga ngurue,na shughuli mbalimbali za ujasiriamali"alisema.


Hongoli aliongeza kuwa watu wenye ulemavu ambao wanaoweza kufanya shughuli ndogo ndogo za kiuchumi wasijinyanyapae na badala yake wajitume.


"Watu wenye ulemavu mmepewa upendeleo mkubwa hata mwenye ulemavu mmoja anaweza kukopa na sisi tunafanya hivyo tunakopesha,kwa hiyo nyinyi wenzetu wenye ulemavu mliopata bahati leo vikundi vichache naomba mkatoe hamasa kwa wenzeni tuone awamu inayokuja,robo inayokuja tupate wenye ulemavu wengi ili kuwainua kiuchumi"alisema Hongoli.


Awali mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Sharifa Nabalang'anya,alisema kuwa mikopo hiyo imetokana na umahiri wa halmashauri ya wilaya ya Njombe kuendelea kuisimamia vyema mianya ya ukwepaji wa mapato ya asilimia kumi, hali ambayo imekuwa ikitoa wasaa wa halmashauri kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato unaosaidia pia mikopo inayotolewa kwa kila robo ya mwaka wananchi walengwa wanaoomba mikopo kupewa kwa wakati.


"Nawaomba mliopata mkopo huu mjitahidi kurejesha kwa wakati ili pia mikopo hii iweze kuwasaidia na waombaji wengine,hatutarajii kuona kikundi kilichopewa mkopo kinashindwa kufikia lengo juu ya manufaa ya kupata mkopo," alisema Sharifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...