Raisa said,Tanga

Suala la kutekeleza watoto ni aina ya unyanyasaji wa jinsia ambayo inaongezeka kuwa tatizo kubwa katika jamii, ingawa katika duru za maendeleo ni suala ambalo bado halipewi kipaumbele cha kutosha. Linachukuliwa poa kwa lugha ya kisasa.

Mkoani Tanga imeelezwa kuwepo na ongezeko la utelekezaji watoto wenye umri wa chini ya miaka saba katika kutokana na sababu mbalimbali jambo linalowafanya watoto hao kukosa ulinzi wa kutosha .

Kwamujibu wa Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoani hapa Mmassa Malugu utelekezaji watoto umeongezeka kutoka mashauri 115 kwa mwaka 2017/2018 hadi kufikia 387 kwa mwaka 2018/ 2019 .

Malugu amesema kuwa mwaka 2016 / 2017 walipokea mashauri 262 kati ya kesi hizo 49 zilipelekwa mahakamani.

Ameeleza kuwa utelekezaji watoto ni miongoni mwa vitendo vya unyanyasaji wanafanyiwa watoto wenye umri huo wa chini ya miaka saba jambo ambalo linawafanya watoto hao kukosa ulinzi na usalama katika makuzi yao..

Hata hivyo, pamoja na kongezeka kwa takwimu za utekelezaji, bado kuna upungufu wa utoaji taarifa za kesi za unyenyesaji na utelekzaji wa watoto kuanzia miaka 0 hadi mitatu.

Kukabiliana na tatizo hilo, Mkoa umeamua kuanzisha kamati za MTAKUWA ambazo zinakuwepo katika ngazi ya vijiji , mtaa , kata halmshauri na Mkoa, kwa ujumla.

Kamati hizo zimeanzishwa ili kusaidia katika malezi, makuzi pamoja na kuhakikisha manyanyaso kwa watoto yanapungua kwa kiasi kikubwa katika maeneo ambayo zipo kamati hizo. Aliongeza kuwa kamati hizo ni mchanganyiko wa watalaam mbalimbali na jamii ambao wanakuwa pamoja .

Mashauri mengi, kama ya vile ya watoto kulawitiwa au kubakwa. yanatokana na wazazi kuacha wajibu wao wa kisheria wa kutunza watoto,” alisema.\

Akizungumzia kuhusu maeneo ambayo vitendo vya unyanayasaji vipo kwa wingi Ofisa huyo alisema kuwa kesi nyingi wanazopokea zinatokea katika maeneo ya Pwani kama vile Mkinga , Pangani na katika shule zilizopo ndani ndani. “Hii inatokana na mifumo tuliyonayo sasa,” alieleza Malugu.

Wataalam wamesema kuwa wakitazama yanayojiri kwa watoto na wanawake yanaonyesha jamii kwa sasa imebadilika sababu mashauri hayo yanatendwa na watu kutoka jamii husika. “Kesi kwa sasa zinaoneka kuongezeka tofauti na awali,” alisema.

Pia alitaja Imani potofu kuhusu watu kutumia watoto kama kafara ya kupata utajiri katika uchimbaji wa madini.

Alitaka jamii kuendelea kushirikiana na kamati zilizoundwa ili kuweza kuwalinda watoto kwa namna moja ama nyingine. Aliwataka viongozi wa dini kuendelea kuzungumza na waumini wao juu ya umuhimu wa malezi na makuzi bora kwa watoto .

Wakizungumza na Mwandishi wa Makala haya baadhi ya Wanawake waliotelekezwa pamoja na watoto wao wamesema jambo hilo linatokana na tamaa walizonazo wanaume pamoja na ulevi uliopindukia .

Mkazi wa Kasera, Jijini Tanga, Husna Shabani Mkazi wa Kasera alidai kuwa ipo haja ya kutoa elimu ya makuzi bora na maendeleo ya mtoto ili kuhakikisha watoto wanalindwa kuanzia wanapozaliwa.

Prisca Mwakasindile, ambaye ni Muuguzi katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu kilichopo Jijini Tanga cha YDCP amesema kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali za watoto wenye ulemavu kutelekezwa na baba zao kutokana na hali zao .

Kwa upande wa baadhi ya Wanaume wamewataka wanaume zao kuacha tabia ya kukimbia majukumu yanayopelekea kumbia familia zao .

Amina Omary Mkazi wa Korogwe amesema kuwa jambo la kutelekeza watoto si jambo jema na hiyo inasabishwa na wazazi kukwepa majukumu yao pamoja na malezi yao wenyewe. Alisema kuna wanaume wamejipa majukumu ya kutafuta watoto lakini bado wao wanakula kwa wazazi wao.

Mzazi mwingine alijitambulisha kwa jina la Hozza Mandia amesema kuwa kinachosababisha watoto kutelekezwa ni migogoro ya kifamilia , kukosekana kwa uaminifu katika mahusiano na hali ngumu za kiuchumi .

Amesema sababu hizo zinapelekea wazazi kutelekeza watoto wao na kuongeza na uzoroteshaji wa makuzi bora ya mtoto, hivyo kufanya mtoto kukosa ulinzi na usalama.

Aidha mpango huo Serikali wa PJT - MMMAM katika vitendo vya ukatili wa watoto kuna upungufu wa utoaji taarifa za kesi za unyanyasaji na utelekezaji watoto kuanzia miaka 0 mpaka minane ambapo kwa utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia katika mkoa wa Katavi umeonyesha asilimia 18 ya wazazi wenye watoto chini ya miaka mitatu kuwapiga vibao watoto wao.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...