Waziri wa Kilimo Hussein Bashe Mei 26,2022 , amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Shirika la Nchi Wazalishaji Kahawa Afrika(InterAfrican Coffee Organization-IACO) Balozi Solomon Rutega, Jijini Nairobi nchini Kenya, wakati wa Mkutano Mkuu wa nchi 25 zinazozalisha Kahawa Afrika,
(G 25 Africa Coffee Summit).

Tanzania na IACO zitashirikiana katika masuala makuu matatu, ikiwa ni pamoja na, Kuanzisha kituo cha ubora cha Kahawa Jijini Dodoma, Kuanzisha kampeni ya unywaji kahawa katika soko la ndani na kuimarisha uhusiano katika Utafiti na Maendeleo ya zao la Kahawa.

“Tanzania itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha makubaliano haya yanatekelezwa kwa ufanisi pamoja na kuendelea jitihada za kukuza tija katika zao la kahawa na kuboresha pato la mkilima” amesema Waziri Bashe

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Balozi Rutega amesema, yuko tayari kutembelea Tanzania na kukutana na wadau katika kutekeleza ushirikiano huu.

Aidha, amepokea pendekezo la Waziri Bashe la Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa tatu, utakaofanyika mwaka 2024.

“Nashukuru sana Waziri kwa ushirikiano wako wa kukuza sekta ya kilimo Tanzania na kubadilisha mtazamo wa sekta ya kilimo kwa vijana, sisi tuko tayari kushirikiana nawe katika jitihada zako za kupambania kukua kwa sekta ya kilimo na hasa zao la kahawa” amesema Balozi Rutega

Waziri Bashe katika mkutano huo ameongozana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao Bw. Nyasebwa Chimagu na Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Bwa Primius Kimaryo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...