*Yashangaa ukimya wao licha ya kupokea fedha nyingi za maendeleo

*CCM yatangaza kuchukua hatua kali dhidi yao, wanafuatilia kwa ukaribu


Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Manyara

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimetoa maelekezo kwa wateule wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiwemo wakurugenzi,wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika Serikali ya Awamu ya Sita.

Kimesema kinashangwa na ukimya uiopo kwa viongozi wa ngazi mbalimbali kushindwa kuelezea mafanikio lukiki ambayo yamekuwa yakifanyika katika maeneo yote nchini hali iliyoelezwa ni kutomtendea haki Rais Samia ambaye ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Akizungumza mbele ya viongozi na Wana-CCM Mkoa wa Manyara leo Mei 14, 2022 ,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho shaka Shamdu Shaka ametumia kikao hicho kuelezea kuwa tangu Rais Samia aingie madarakani amefanya kazi kubwa na nzuri ya kuwatumikia wananchi ikiwa pamoja na kupeleka maendeleo lakini cha kushangaza hakuna anayesema, wamekaa kimya.

“Tunayo kazi wana CCM kuunga mkono juhudi hizi ambazo viongozi wetu wakiongozwa na Rais Samia ambaye ni Mwenyekiti wetu Taifa, kazi kubwa inafanyika na bahati mbaya sana Serikali ya CCM inatoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu lakini bado kumekuwa na ukimya wa kusema juhudi hizi zinazofanywa na Serikali, kila mmoja anayo dhamana ya kuisema serikali.

“Kila mmoja aseme kazi kubwa na nzuri inayofanywa, ili kuzima proganda ambazo zinatolewa na kikundi ambacho kiko mtandaoni ambacho kazi yake ni kueneza propaganda chafu.Nitoe mwito kwa wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya,wakurugenzi na viongozi wote ambao ni wateule wa Rais kote nchini watambue wanayo nafasi ya kusema mafanikio ya serikali.

“Wamekuwa kimya hawasemi utadhani wamepigwa ganzi, hawamtendei haki Rais , hivyo ni vema kwanza wakamuunga mkono, pili wakasemea maendeleo.Nimefanya utafiti huko nyuma miaka miwili iliyopita ulikuwa ukikaa kwenye televisheni utaona wakuu wa wilaya au wakuu wa mikoa zaidi ya watatu au wa wanne wanazungumzia mafanikio ya Serikali,”amesema Shaka ambaye pia ni Mlezi za CCM mkoa wa Manyara.

Ameweka wazi kutokana na mwenendo huo , CCM inafanya tathmini kufuatilia utendaji kazi kwa viongozi hao waliopewa dhamana na kuaminiwa na Rais lakini wamekuwa kimya kwa kutozungumza chochote kinachohusu mafanikio licha ya kupelekewa fedha nyingi za maendeleo.

“Kwanini miaka miwili viongozi hao wawe wanasema kuhusu mafanikio na sasa watu hawasemi.Tutachukua hatua.Narudia tena kusisitiza kazi kubwa imefanyika na kila mmoja ni shuhuda,hivyo ni lazima tuiembe wimbo mmoja.Huku wilayani kuna viongozi na kuna maendeleo yanafanyika lakini wanasubiri hadi aje Rais Samia ndio aseme wakati viongozi wako kwenye maeneo hayo, tubadilike ndugu zangu,”amesema Shaka.

Akizungumza zaidi ,Shaka amewahakikishia Watanzania kwamba Rais Samia atatuvusha bila wasi wasi wowote, ataivusha nchi kwa uthubutu wake,maoni yake, kwa dira aliyojiwekea na ataivusha nchi kwa kutekeleza Ilani ya CCM kwa asilimia 100

“Wote ni mashahidi ndani ya mwaka mmoja Rais Samia ameongeza lakini mafanikio ambayo yamepatikana katika Nyanja mbalimbali utadhani ameongoza miaka mitano, Rais Samia ameifungua nchi kiuchumi, amefungua diplomasia ya nchi hii, leo Tanzania imerudi kwenye ramani.Hakuna asiyeijua Tanzania na yeye ndio kinara wa demokrasia na diplomasia ya kiuchumi.

“Niwaombe sana wana CCM puuzeni wale wote wenye nia uovu ya kufifisha yale yote yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita, wamekuwepo watu wachache mtandaoni wamekuwa wakibeza.Rais Samia ataivusha Tanzania na atakivusha Chama Cha Mapinduzi.”


Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Shaka Hamdu Shaka, akizungumza katika Mkutano wa Ndani wa Viongozi na Wanachama wa CCM Katika Wilaya za Babati Mjini Na Vijijini katika Ziara yake ya Kukagua Uhai Wa Chama Mkoani humo.
Wanachama Mbalimbali wakinyanyua Vipeperushu Juu wakati wa Mkutano wa Ndani wa Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Taifa  Shaka Hamdu Shaka,pamoja na Viongozi na Wanachama wa Mkoa wa Manyara
Wanachama Mbalimbali wakifutailia kwa makini yaliyokuwa yakijiri wakati wa Mkutano wa Ndani wa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Taifa Shaka Hamdu Shaka,pamoja na Viongozi na Wanachama wa Mkoa wa Manyara


Wanachama Mbalimbali wakinyanyua Vipeperushu Juu wakati wa Mkutano wa Ndani wa Katibu CCM wa Itikadi na Uenezi Taifa  Shaka Hamdu Shaka,pamoja na Viongozi na Wanachama wa Mkoa wa ManyaraWanachama Mbalimbali wakifutailia kwa makini yaliyokuwa yakijiri wakati wa Mkutano wa Ndani wa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Taifa Shaka Hamdu Shaka,pamoja na Viongozi na Wanachama wa Mkoa wa Manyara


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...