Na. John Mapepele

Katibu Mkuu wa Utamadun,Sanaa na Michezo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kuitangaza Tanzania kupitia Royal Tour. Dkt, Hassan Abbasi amesema filamu hiyo ni lango linalokwenda kufungua maendeleo kwenye kila sekta hapa nchini.

Akizungumza leo Mei 13, 2022 kwenye Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali jijini Tanga. Dkt, Abbasi ametoa wito kwa Maafisa Habari kuitangaza  na amemkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali nakala ya filamu hiyo ili isambazwe nchini kupitia kwa maafisa hao.

Akitaja baadhi ya faida ya filamu hiyo amesema inakwenda kutazamwa na zaidi ya watu bilioni moja katika kipindi kifupi.

Aidha, amesema katika uzinduzi uliofanywa nchini Marekani ambako ni soko kuu la utalii wa Tanzania ameweza kukutana na viongozi matajiri namba moja katika sekta mbalimbali ambao wameonyesha nia ya kuwekeza hapa nchini.

Ameongeza kuwa filamu hiyo ya kihistoria,  imetengenezwa katika kiwango cha kimataifa na wataalam nguli duniani ambao pia wanamitandao mikubwa  ya kuisambaza.

Ametumia fursa hiyo kumpongeza  Mhe. Rais kwa kazi kubwa aliyofanya na kuwaomba maafisa Habari na watanzania kwa ujumla  kumwombea katika kazi kubwa anayoifanya ya kuitangaza na kufungua Tanzania duniani ili kuvuta wawekezaji na watalii nchini.

"Nampongeza Mhe. Rais kwa kushiriki moja kwa moja katika kuitengeneza filamu hii haikuwa kazi rahisi" amesisitiza Dkt. Abbasi

Kauli mbiu ya kikao hicho ni " Mawasiliano ya Kimkakati nyenzo muhimu kufanikisha  sensa ya Watu na Makazi 2022"

Kikao kazi hicho kimefungwa rasmi na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Lugha Bashungwa ambaye amesisitiza Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kusemea mafanikio ya Serikali.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...