Na Pamela Mollel,ARUSHA

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Kanda ya Kaskazini imepiga mnada wa wazi wa madumu 170 yenye lita 250 kila moja za kemikali aina ya Ethly na kupata Sh.milioni 68 zitakazolipwa na Kampuni ya Rastonty Enterprises Ltd ya Moshi mkoani Kilimanjaro iliyoshinda mnada huo.

Akizungumza jijini Arusha baada ya mnada huo kumalizika,Mkuu wa Kitengo cha Huduma za sheria GCLA, Gilbert Ndeoruo alisema, mshindi wa mnada huo ameshinda kwa kukubali kununua kila dumu moja kwa Sh.400,000 ambazo anatakiwa kulipa asilimia 25 ya fedha zote na inayobaki atamalizia ndani ya siku 14.

Alisema madumu hayo yalipatikana mwaka jana baada mfanyabiashara mmoja(hakutajwa jina) kukamatwa akiingiza Madumu hayo kinyume na serikali bila kuwa na vibali vya GCLA.

"Sisi tulimkamata na kumfikisha mahakamani na tulishinda kesi kwa mahakama kuamuru madumu haya kutaifishwa na serikali baada ya kubaini muhusika aliingiza nchini kinyume na sheria na leo tumepiga mnada na kupata fedha hizi,"alisema

Alisema muhusika wa madumu hayo amepata hasara kwa sababu ya kukiuka sheria za mamlaka hiyo, yenye jukumu la usimamizi na udhibiti wa kemikali za majumbani na viwandani ambayo pia imepewa dhamana ya kusimamia matumizi ya kemilikali nchini na watu wote wanakingiza bidhaa hiyo,kutumia au kuhifadhi lazima watambulike kwao na wawape mafunzo.

Alitoa wito kwa watu wote wanataka kufanya biashara hiyo,wahakikishe wanafika kwenye ofisi hizo ili wapewe utaratibu na elimu,kwa ajili ya kuwasaidia kuepuka hasara pale wanapoingia kwenye mikono ya serikali kwa kufanya biashara hiyo kinyume cha sheria na kuhatarisha afya za watu na mazingira.

Meneja wa GCLA Kanda ya Kaskazini,Christopher Anyango,alisema kazi yao kulinda kemilikali zote zinazoingia nchini,sababu zisipotumika vyema inaleta athari kwenye afya na mazingira.

"Hivyo lazima sisi tuwasajili na kukagua pamoja na kutoa vibali na elimu, tunaamini anayesajili atakuwa amelazwa namna salama ya kutumia kemikali hii,ili kutoleta athari za afya na mazingira na hii ni mojawapo ya matumizi ya viwandani,tusipodhibiti inaweza leta athari kubwa katika maeneo hayo,"alisema

Alisema kemikali hiyo imenunuliwa kwa ajili ya kwenda kusaidia kutengeneza vinywaji vya pombe kali na isipotumika Kwwnye hiyo kazi ilivyokusudiwa ikatumika maeneo mengine inaweza kusababisha madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo kuleta upofu ba kuharibu mapafu.

Kwa upande wake mashindi wa mnada huo ambaye pia ni mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni ya Rastonty Enterprises LTD ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Joyce Mugendi aliiahukuru serikali kwa kutangaza mnada huo na kufanya kwa haki na uwazi.

"Sisi Leo tumeshimda kwa kununua dumu moja Sh.400,000 ambapo leo tumelipa asilimia 25 ya fedha zote kama sheria inavyotaka na ndani ya siku 14 tutamaliza fedha yote tunayotakiwa kulipa na sisi kwa kemilikali hii tunaenda kuuzia wanatengeneza pombe kali za aina mbalimbali wanaotambulika na serikali na siyo vinginevyo,"alisema.
Meneja wa mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kanda ya kaskazini (GCLA)Christopher Anyango akizungumza na waandishi wa habari juu ya mnada huo
Mshindi wa mnada huo kutoka kampuni ya Rostonty Enterprise LTD ya Moshi mkoani Kilimanjaro Joyce Mugendi alieleza kuwa mnada huo umeendeshwa kwa haki

Madumu 170 yaliyo na kemikali yaliyouzwa kwa mnada jijini Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...