Na Pamela Mollel,Arusha

Mawakili wa serikali wametakiwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika majukumu yao badala yake kuwa waadilifu katika utendaji wao

Rai hiyo ilitolewa na Waziri wa katiba na sheria Drt Damas Ndumbaro jijini Arusha wakati akifunga mafunzo ya siku nne kwa mawakili zaidi ya 600 waliopewa mafunzo kupitia ofisi ya wakili mkuu wa serikali.

Drt Ndumbaro amesema kuwa endapo watajihusisha na rushwa watambue wazi kuwa rushwa haina siri na matendo yake yataanza kuonekana

"Rushwa ni adui wa haki lazima tuepuke kwa nguvu zote,unapoamua kuchukua rushwa lazima matendo yako yataanza kuonekana"alisema Drt Ndumbaro

Amewataka mawakili kutambua kuwa Wana wajibu wa kuheshimu sheria ikiwa ni pamoja na kusaidia Taasisi za serikali katika maswala ya kisheria

Drt Ndumbaro ameongeza kuwa mafunzo hayo ni ya kipekee na ni fursa kubwa kwa mawakili kubadilishana uzoefu

Aidha amewataka kuhakikisha mafunzo waliyoyapata yanakuwa Chachu ya utatuzi wa migogoro.

Kwa upande wake Wakili mkuu wa serikali Gabriel Malata akitoa hotuba yake kwa waziri amesema kuwa pamoja na mafanikio lakini bado Wana changamoto ya mawakili kutopata mafunzo maalum yanayoendana na uchumi wa Sasa

Malata ameongeza kuwa baada ya mafunzo hayo mawakili hao wameiva na wataleta Chachu katika kuhakikisha maslai ya taifa yanalindwa ipasavyo.

Akitoa shukrani kwa niaba ya mawakili walioshiriki mafunzo hayo wakili Yesaya Mahenge kutoka mkoani Singida amesema kuwa mafunzo waliyoyapata juu ya namna yankuwndesha mashauri na mengineo yatawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi na kuahidi kuwa ni hazina kubwa waliyoipata

Katika mafunzo hayo washiriki 600 kutoka taasisi 114 za kiserikali na wizara wameshiriki katika mafunzo hayo.



 Waziri wa Katiba na sheria Dkt Damas Ndumbaro akizungumza katika mafunzo ya mawakili wa serikali yaliyofanyika jijini Arusha

Wakili Mkuu wa serikali Gabriel Malata akizungumza katika mafunzo ya mawakili jijini Arusha
Baadhi ya mawakili wa serikali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...