Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

RAIS wa Heshima na Mwekezaji katika Klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji (MO Dewji) Mei 20, 2022 siku ya Ijumaa, ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa heshima na Shule ya Biashara ya McDonough ya Chuo Kikuu cha Georgetown mjini Washington nchini Marekani.

Kupitia tuvuti rasmi ya Chuo hicho, MO Dewji amezungumzia umuhimu na wajibu wa kuinua wengine na kujitoa kwa jamii inayomzunguka, amewaasa Watahiniwa wenzake kujitoa na kurudisha kwa jamii zinazowazunguka.

“Sina shaka na nafasi zenu za juu, lakini nawaasa katika nafasi hizo, mkumbuke kurudisha kwa jamii kile kinachopatikana kwenu", amesema MO Dewji.

MO Dewji ameona umuhimu kurudisha kwa jamii akikumbuka tukio la kutekwa nyara zaidi ya wiki, ambapo jamii hiyo ilipaza sauti ili kuachiwa huru, sauti hizo zilipazwa kupitia marafiki, ndugu wa karibu, mitandao ya kijamii na hata vyombo mbalimbali vya habari.

Amesema jamii inayomzunguka imefanya mema kwake hivyo hana budi kurudisha kwao. "Kama umepata maarifa ukiwa hapa, hakikisha maarifa hayo unayatumia vizuri, hakikisha unaondoa uoga na kuacha urithi mzuri kwa jamii yako inayokuzunguka.

MO Dewji ambaye ni Rais wa Makampuni ya MeTL Group na Mwanzilishi wa Mo Dewji Foundation ametunukiwa Shahada hiyo ya Udaktari wa heshima katika Mahafali hayo na Rais wa Chuo hicho, John J. DeGioia.

Rais wa Heshima na Mwekezaji katika Klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji (Kushoto) akipongezwa na Rais wa Chuo Kikuu cha Georgetown, John J. DeGioia (Kulia) baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa heshima na Shule ya Biashara ya McDonough ya Chuo hicho.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...