Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ameongoza ujumbe wa Tanzania kuhudhuria katika Tamasha la Utalii wa Utamaduni la kutangaza vyakula vya asili lililoandaliwa na Serikali ya Zimbabwe, lililofanyika kwenye viwanja vya hoteli ya Elephant Hills katika eneo la Victoria Falls nchini Zimbabwe.
Akizungumza baada ya tamasha hilo Mhe. Masanja amesema tamasha hilo ni fursa ya kipekee ya kutangaza Utalii wa Utamaduni kupitia vyakula vya asili hivyo Tanzania inaweza kuiga mfano huo wa kutangaza vyakula vya asili ili kuvutia watalii wengi zaidi.
Mhe. Masanja ameshiriki katika kutembelea mabanda ya washiriki ambao ni wazawa wa Zimbabwe, akiwa ameongozana na Mke wa Rais wa Zimbabwe, Dkt. Amai Auxillia Mnangagwa pamoja na Mawaziri wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii, Mazingira, Maliasili na Utalii kutoka nchi za Zambia, Namibia na Botswana, na kisha kushiriki katika zoezi la kugawa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.
Mhe. Masanja yupo nchini Zimbabwe kwa ajili ya kushiriki kwenye Kongamano la Tembo wa Afrika litakalofanyika katika Hifadhi ya Taifa Hwange ikiwa na lengo la kuunda mpango mpya na bora zaidi wa uhifadhi wa Tembo na kukuza Utalii Barani Afrika.







 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...