Na Mwandishi wetu

Kampuni ya Kimataifa ya huduma ya Kontena Tanzania (TICTS) imendelea kuleta ufanisi katika shughuli zake baada ya kuleta mashine tatu za kutoa huduma ya ushushaji na kupandishaji wa makontena zijulikazo kwa jina la Rubber-Tyred Gantry Cranes (RTGCs).

Mashine hizo za kisasa zinatumia na matairi zimenunuliwa naTICTS kwa lengo la kuendelea kutoa huduma bora zaidi za kontena ikiwa pamojana mpango unaoendelea wa uwekezaji ambapo kampuni hiyo imewekeza Sh12.5 billioni katika kununua vifaa hivi vya ziada.

Hivi karibuni, TICTS ilivunja rekodi ya kuhudumia jumla mizigo 61, 000 ya makontena yenye ujazo wa futi 20 (TEU) kwa mwezi Machi na jumla ya TEU 2,841 mnamo mwezi huu (Mei).

Mkurugenzi Mkuu wa Hutchison Ports Andy Tsoi, alisema kuwa wanaendelea kunufaika katika shughuli zao na kuendelea kutoa huduma bora kwawateja wao.

“Kama mwanachama wa Bandari za Hutchison, TICTS inaendelea kunufaika kutokana na kupata usaidizi mbalimbali kutoka makao makuu ya kampuni yetu. Tuna historia kubwa ya ushirikiano nchini Tanzania na tunatamani sana kuendelea kusaidia ukuaji wa Tanzania na ukanda huu,” alisemaTsoi.

Akizungumzia ujio wa vifaa hivyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TICTS Matt Clifftn alisema kuwa, “Kulingana na kuendelea kukua kwa uchumi, tunayofuraha kupokea vifaa hivi vya ziada kwani vitatusaidia kukidhi mahitaji katika kutoa huduma bora. Lengo letu ni kupunguza muda wa meli kusubiri na kuongeza tija.”

TICTS ipo katika sehemu ya gati Nane(8)8 hadi 11, eneo lenye urefu wa mita 725 bandarini ikiwa na ‘crane’ sita kila moja ikiwa na uwezo wa kubeba tani 45.

Pamoja na kuwasili kwa vifaa, TICTS kwa sasa kina idadi ya mashine za RTGC 23 ambazo zinafanya kazi katika eneo la hekta 18.75.


Mashine tatu za kutoa huduma ya ushushaji na kupandishaji wa makontena zijulikazo kwa jina la Rubber-Tyred Gantry Cranes (RTGCs) baada ya kuwasili nchini kupitia kampuni ya Kimataifa ya huduma ya Kontena Tanzania (TICTS)


Mashine tatu za kutoa huduma ya ushushaji na kupandishaji wa makontena zijulikazo kwa jina la Rubber-Tyred Gantry Cranes (RTGCs) katika muonekano tofauti baada ya kuwasili nchini kupitia kampuni ya Kimataifa ya huduma ya Kontena Tanzania (TICTS)


Mashine tatu za kutoa huduma ya ushushaji na kupandishaji wa makontena zijulikazo kwa jina la Rubber-Tyred Gantry Cranes (RTGCs) katika muonekano tofauti baada ya kuwasili nchini kupitia kampuni ya Kimataifa ya huduma ya Kontena Tanzania (TICTS)



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...