Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson (kushoto) na Waziri wa Nishati January Makamba (kulia) walipotembelea banda la PURA kwenye Maonesho ya Majukumu ya Wizara na Taasisi Zake, yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.




Na Janeth Mesomapya

WABUNGE na viongozi mbalimbali wa Serikali wanatarajiwa kuelimishwa kuhusu Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) na shughuli inazozitekeleza kwenye Maonesho ya Majukumu ya Wizara ya Nishati na taasisi zake.

Maonesho hayo yaliyoanza rasmi leo, Mei 23, 2022 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma yanaongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Nishati kwa Maendeleo Endelevu’ na yatafikia tamati Mei 26, 2022.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba, maonesho hayo yanalenga kujibu maswali ya wabunge juu ya masuala mbalimbali ya sekta ya nishati na kutatua changamoto mbalimbali zinazohusiana na sekta.

Wataalamu wa PURA wamejipanga kuongeza uelewa kwa wabunge hao kwa maeneo mbalimbali ikiwemo ya mradi wa kubadili gesi asilia kuwa kimiminika (LNG), ushiriki wa wazawa kwenye miradi mbalimbali ya sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia pamoja na fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye utekelezaji wa miradi ya mkondo wa juu wa petroli.

Mjiolojia Ebeneza Mollel ameeleza kuwa maonesho haya ni jukwaa muhimu kwa PURA kuwafikia wananchi kupitia viongozi wao kwa kuwaongezea uelewa na namna bora ya kutumia fursa zinazopatikana katika utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya mafuta na gesi asilia.

“Viongozi hawa ni kundi muhimu kufahamu fursa hizi kwani wanaweza kufikia wananchi kwa urahisi zaidi ikiwa ni pamoja na kuwasaidia na kuwajengea uwezo wa jinsi ya kuchangamkia fursa hizi,” alieleza.

Naye Mjiolojia Wangese Matiko amebainisha kuwa wabunge watakaotembelea banda la PURA pia watapata fursa ya kujifunza masuala ya kiufundi kama ya mnyororo wa thamani wa mafuta na gesi asilia, shughuli za utafutaji na uzalishaji zinazoendelea nchini na mengineyo.
Wajiolojia wa PURA, Ebeneza Mollel (kulia) na Wangese Matiko (katikati) wakitoa elimu kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia kwa moja ya washiriki waliotembelea banda la PURA kwenye Maonesho ya Majukumu ya Wizara na Taasisi Zake, yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.
Wajiolojia wa PURA, Ebeneza Mollel (kulia) na Wangese Matiko (katikati) wakitoa elimu kuhusu sekta ya mafuta na gesi asilia kwa moja ya washiriki waliotembelea banda la PURA kwenye Maonesho ya Majukumu ya Wizara na Taasisi Zake, yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.
Wajiolojia wa PURA, Wangese Matiko (kushoto) na Ebeneza Mollel (kulia) wakifafanua jambo kwa moja ya washiriki waliotembelea banda la PURA kwenye Maonesho ya Majukumu ya Wizara na Taasisi Zake, yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...