Wahitimu wa Mahafali ya tano ya Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) wakiwa na vyeti vyao mara baada ya kutunukiwa vyeti vyao katika Ukumbi wa Mlimani City jiji Dar Es Salaam, Mei 13, 2022.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi akitunuku Cheti mmoja ya Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi leo Mei 13, 2022 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wahitimu wakisikiliza viongozi mbalimbali wakati wa Mahafali yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salaam leo Mei 13, 2022.

Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi katika Taasisi ya Uongozi wakiingia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salaam leo Mei, 13 Wakati wa mahafali ya tano ya wahitimu wa Diploma ya uongozi na ngazi ya cheti cha Uongozi.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
SERIKALI imesema inamatuimaini makubwa na viongozi mbalimbali ambao wamehitimu mafunzo ya Stashahada ya Uzamili ya Uongozi pamoja na mafunzo ya uongozi kwa njia ya mtandao kwa ngazi ya cheti yanayotolewa na Tasisi ya Uongozi ikishirikiana na chuo cha Aalto EE cha Nchini Finland 

Akizungumza wakati wa mahafali ya wahitimu hao yaliyofanyika Mliman City ,Naibu Waziri, Ofisi ya Rais , Utumishi na Utawala Bora Deogratius Ndekembi amesema serikali inatamani kuona baada ya kumaliza mafunzo sasa  kuonesha kile walichojifunza  kinaoneshwa kwa vitendo.

“Tunataka  kuona  uongozi wa kimkakati tunataka, tunataka kuona mnasimamia   vizuri rasilimali watu na rasilimali fedha, tunataka kuona mboresha  nyanja ya mawasiliano na mahusiano baina  yenu nyinyi kama watumishi wa umma lakini pia mawasiliano na mahusiano baina yenu na wadau wengine wa masuala ya maendeleo ndani na nje ya nchi yetu.

Amesema Nchi ya Tanzania  imejaliwa rasilimali mbalimbali, Madini, Mito, Bahari, mimea na nyinginezo na ili rasilimali hizi ziwe na manufaa kwa taifa lazima kuwe na rasilimali watu wenye weredi wa kutosha hivyo mafunzowaliyoyapata ni sehemu ya kuwajengea uwezo kwaajili ya kusimamia raailimali zetu kikamilifu kwa mstakabali wa taifa.

"Kiongozi mzuri ni yule anayewajibika na kutekeleza majukumu yake bila kushurutishwa....." amesema  Ndejembi na kuongeza mategemo ni kusoma utumishi bora, wenye msingi imara na thabiti kiuongozi na kiutendaji mara baada ya kurejea sehemu za kazi wahitimu hao wa mahafali ya tano.

Aidha amewakaribisha rasmi washiriki wa awamu ya sita katika mafunzo ya uongozi, " Matumaini yangu washiriki wapya mtafuata nyayo za wenzenu na ikiwezekana mfanye vizuri zaidi ili muache alama, nawasihi mtoe ushirikiano mzuri kwa waendeshaji wa mafunzo hayo..." Amewaasa ndejembi

Amewaomba Taasisi ya Uongozi kuandika tawasifu ya Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho kikwete na  Rais wa awamu ya tano, Hayati Dkt. John Magufuli,
lakini pia amewapongeza
 kwa kwa kuandika tawasifu za viongozi wa awamu ya pili na tatu.

Kwa upande wa Katibu Mkuu Kiongozi Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said amewaasa viongozi kutokuwa wabinafsi pale zinapotokea fursa mbalimbali katika jamii.

"Wengine wanakuwa wanajali  wa Kwao na Jamaa zao.. wengine husema kutesa kwa zamu kwakuwa mwezao yupo juu pale..., hivi hatakiwi kwa kiongozi..." Amesema Injinia Zena

Amesema viongozi wengine wanafikilia kuwa Uongozi ni kama ajira ya kwaida na kupata mshahara wake, lakini dhima kubwa ya Uongozi ni kuonesha njia kwa wengine mfano mahali popote penye  kiongozi panatakiwa kujulikana kama yupo.

Amesema kiongozi anatakiwa kuwa kuwatia moyo wengine walio chini yake ili waweze kuendeleza vipaji vyao, sio kuwavunja moyo au kuwa na kauli za kudharau na kukatisha tamaa katika kazi na jitihada wanazojaribu kuonesha mahali pa kazi. 

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute,) Dkt. Kadari Singo amesema, Taasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuandaa na kuendesha mafunzo kwa viongozi, kuendesha majadiliano ya kisera na kufanya tafiti za kisera, kutoa ushauri wa kitalaam na kuzisaidia taasisi mbalimbali pamoja  na viongozi wake katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute,) ilianzishwa Julai, 2010 kwa malengo ya  kuwa na kituo cha utalaam wa juu cha kuendeleza viongozi barani Afrika kwa kuanzia nchini Tanzania, Kanda za Afrika Mashariki na hatimaye Afrika nzima.

Katika Mahafali ya tano ya Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) jumla ya wahitimu 41 wamefunzu Stashahada ya Umahili ya mafunzo ya Uongozi na mafunzo kwa njia ya mtandao kwa ngazi ya  Cheti cha Uongozi 76 wamefunzu na kutunukiwa vyeti vyao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...