Katibu Tawala wa Mkoa Dar es Salaam Hassan Rugwa amesema Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) imetoa suluhu ya usafiri kwa maalum katika kipindi cha maonyesho ya biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba).

Rugwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati uzinduzi wa safari maalum mabasi yaendayo haraka katika maonesho ya sabasaba kwani imerahisisha usafiri kwa wananchi pamoja na wafanyabiashara kwa kipindi cha sabasaba.

Amesema huduma ya usafiri ni changamoto katika kipindi cha maonesho hivyo DART imeona hilo mbalimbali katika kusaidia wananchi kupata usafiri wa uhakika wakiwa katika maonesho.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Deus Kasmir amesema DART imejipanga katika kutoa huduma ya usafiri katika kipindi cha maonesho ya sabasaba kwani wanatambua idadi kubwa ya ambao wanahitaji kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Amesema katika hiki wananchi wanaokwenda katika maonesho ya sabasaba wasifikiri suala la usafiri kwani usafiri upo katika safari za mbagala hadi viwanja vya sabasaba na Gerezani Sabasaba .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Hassan Rugwa Katikati wa mbele akiingia katika viwanja sabasaba kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Latifa Khamis na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DART Deus Kasmir
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Hassan Rugwa akihakikiwa tiketi yake ya Safari tayari kwa ajili ya kuzindua huduma maalum ya Mabasi yaendayo haraka kuelekea viwanja vya Maonesho Mwalimu J.K Nyerere (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Hassan Rugwa akiwa katika picha ya pamoja Wafanyakazi wa DART na Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...