VIONGOZI wa dini mbalimbali nchini kupitia Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania wamepongeza mchakato unaondelea wa wakazi walioko hifadhi ya Ngorongoro kuhama kwa hiyari na wao wameridhishwa na hatua ambazo Serikali imezichukua katika kusimamia mchakato huo.

Akizungumza leo Juni 30,2022 kwa niaba ya kamati hiyo na Jumuiya ya maridhiano ,Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema viongozi wa dini kwa umoja wao wamefika Ngorongoro eneo ambalo wananchi wanahama kwa hiyari yao.

“Lengo letu la kuja hapa ni kutaka na kuona Serikali inawafanyia nini wananchi hawa,

Je kuna malalamiko gani, kuna shida gani , lakini tumefika hapa tumeona wananchi wanaanza kuhama kwa hiyari zao wenyewe na wale wachache waliobaki wanaendelea kujiandikisha bila bughudha yoyote ili kutekeleza yale ambayo Serikali inayataka.

“Lakini Serikali imefanya hivi kwa nia njema kwa maslahi mapana ya nchi lakini hata maelezo tuliyopokea kutoka kwa wasimamizi wa mchakato huu kule wanakohamia Msomera wilayani Handeni kuna mazingira mazuri zaidi kuliko haya.Tumeona hapa mazingira si sawa na yale kule wanakohamia, ni kuzuri zaidi kimaisha,”amesema Sheikh Alhad.

Ameongeza anaamini kule wanakohamia watapata maisha mazuri, kwanza wametengewa mazingira mazuri, kuna shule, hospitali na nyumba zinaendelea kujengwa kwa hiyo kuhama huko kwa hiyari kuna tija nzuri ambayo wananchi wanakwenda kuipata.“Leo wenyewe tumewaaga wale wanaokwenda Handeni na tumewaaga wakiwa na furaha,hakuna aliyelazimisha , wote wanaondoka kwa hiyari yao wenyewe.

“Kwa hiyo wale wanaojaribu kuchafua taaswira ya nchi ni vizuri wakatuacha na Serikali yetu ya Awamu ya Sita ya Mama Samia Suluhu Hassan, watuache na Serikali yetu inayofanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kuchunga maslahi ya wananchi wake, hatutaki kuingiliwa kwani hii ni nchi yetu.

“Na hawa wanaohama kwa hiyari ni watanzania ambao wako chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hiyo kutii mamlaka zao ni jambo ambalo ni lalazima lakini kwa hiyari .Wanatii mamlaka kwa hiyari na watii mamlaka katika jambo jema kwani inawatoa katika mahala ambapo si salama kuwapeleka mahala salama zaidi,”amesema Sheikh Alhad.

Ameongeza kwa hiyo wao viongozi wa dini wanaishukuru Serikali kwa kusimamia mchakato huo kwa namna ambayo kwa hakika Rais atafurahia kwani hakuna kilio cha mtanzania na mchakato umekwenda kwa uzuri kabisa.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Angilikana Dar es Salaam Jackson Sosteness Jackson ambaye pia ni Katibu wa Kamati za Amani ametoa pongezi kwa Serikali kwa namna ambavyo imeweza kuliweka jambo hilo pamoja na kujali maslahi mapana ya rasilimali za nchi lakini utu wa watu umethaminiwa na kuheshimiwa katika hali ya juu.

“Hayo yamedhihirika katika namna ambavyo Serikali imeweza kusimamia katika mambo mbalimbali ikiwemo mazingira ya kuondoka kwao lakini mazingira ya wakazi hawa watakayokwenda kukutana nayo kule na hasa katia kuweka fidia na huduma mbalimbali ili kuweza kuyakabili maisha katika mazingira mapya.Kwa hiyo niipongeze Serikali kwa kuanzia na Rais wetu,”amesema Askofu Jackson.

Amesema Serikali imefanya kazi kubwa iliyoambatana na utu ambao Mungu ameuweka kwa watendaji wote ambao wamekuwa wakisimamia mchakato huo .Aidha amewapongeza wakazi wanaohama kwa kuonesha uzalendo wa hali juu, jambo ambalo hata kama kuna sauti nyingi bado wametoa ushirikiano na shuhuda ambazo zimetolewa zinaeleza wazi ni kwa namna gani suala hilo wamelipokea.

Wakati huo huo Mjumbe wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania ambaye pia Laigwanani Mkuu anayefanya kazi katika Baraza la Maraia Esack Ole kisongo Meijo amesema wakazi wa maeneo hayo wanahama kwa hiyari kwenda Msomera na yeye ameshuhudia kwa jicho lake.

“Waziri wa Maliasili na Utalii nikupongeze sana kwa maandalizi mazuri kwa niaba ya Serikali, lakini mkuu wangu wa Mkoa John Mongella Mungu amekujaalia sana , katika hili mwaka huu wote umesimama imara kuhakikisha watu wa Ngorongoro wanapata haki zao za msingi lakini jamii ya wamasai wasiingiliwe na kusumbuliwa.

“Umefanya vikao mbalimbali vya kuhamasisha mpaka umeeleweka , wengine hawajafahamu mambo ambayo yamefanywa na mkuu wa mkoa, mimi nafuatilia na ninaishi mkoa huu wa Arusha.Nikupongeze na nikupe pole kwani umepunguza kilo lakini umehakikisha nchi inakuwa salama na hifadhi zetu zinatunzwa na kuendelezwa.

“Umeelimisha watu , nampongeza Rais wetu kwa kuwa mvumilivu na mnyenyekevu kwa ajili ya wananchi wake , amehakikisha kila mtu anapata haki za msingi. Amekuwa hodari wa kufuatilia na anahakikisha elimu inafika kwa watu.Niwapongezee wakazi wa Ngorongoro kwa uamuzi huu.Kule Msomera ni nchi ya tambarare inaasali na maziwa ni kama Mungu aliwawekea.”

Viongozi wa Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano wakiwaaga 
kundi la tatu la kaya 25 za wananchi wanaohama kwa hiyari kutoka katika hifadhi ya Ngorongoro kwenda kijiji cha Msomera, Handeni mkoani Tanga   kupisha shughuli za uhifadhi katika eneo la Ngorongoro.




Viongozi wa Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano wakiwa wamefika kutembelea moja ya kijiji cha Kimba ndani ya hifadhi ya Ngorongoro ambako walikuwaa wakiishi wakaazi katika eneo hilo na baadae kwa hiyari yao kuamua kuhama kupisha shughuli za uhifadhi na kuelekea katika kijiji cha Msomera,Handeni mkoani Tanga.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-NGORONGORO


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana alipokuwa akiwapokea viongozi wa Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano katika ofisi za hifadhi ya Ngorongoro,waliofika kwa ajili ya kuwaaga Wakaazi waliokuwa wakiishi katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro ambao tayari kwa hiyari yao wameamua kuhamia Msomera,Handeni Tanga

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana alipokuwa akiwapokea na kuwakaribisha viongozi wa Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano katika ofisi za hifadhi ya Ngorongoro,waliofika kwa ajili ya kuwaaga Wakaazi waliokuwa wakiishi katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro ambao tayari kwa hiyari yao wameamua kuhamia Msomera,Handeni Tanga .Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongera akisalimiana na mmoja wa viongozi wa kamati ya Amani na Maridhiano.
PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-NGORONGORO
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Jumuiya ya maridhiano ,Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akizungumza jambo wakati kuwaaga Wakaazi waliokuwa wakiishi katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro ambao kwa hiyari yao wameamua kuhamia Msomera,Handeni mkoani Tanga


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana leo Juni 30,2022 akishiriki zoezi la kuaga kundi la tatu la kaya 25 za wananchi wanaohama kwa hiari kutoka katika hifadhi ya Ngorongoro kwenda kijiji cha Msomera, Handeni mkoani Tanga kwa kuwakabidhi hati za malipo ya fidia.

PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-NGORONGORO viongozi wa Kamati ya Amani na Jumuiya ya Maridhiano wakiwa katika ofisi za hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuaga kundi la tatu la kaya 25 za wananchi wanaohama kwa hiari kutoka katika hifadhi ya Ngorongoro kwenda kijiji cha Msomera, Handeni mkoani Tanga

 Baadhi ya kundi la tatu la kaya 25 za wananchi wanaohama kwa hiari kutoka katika hifadhi ya Ngorongoro kwenda kijiji cha Msomera, Handeni mkoani Tanga wakiagwa

 Mjumbe wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania ambaye pia ni Laigwanani Mkuu anayefanya kazi katika Baraza la Maraia Esack Ole kisongo Meijo amesema wakazi wa maeneo hayo wanahama kwa hiyari kwenda Msomera na yeye ameshuhudia kwa jicho lake.
 .




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...