Shirika la Posta Tanzania na Kampuni ya Usafirishaji (TUTUME) wamesaini mkataba wa makubaliano ya kushirikiana kibiashara unaolenga kurahisisha na kuimarisha upatikanaji wa huduma za Afya nchini, huku ukishuhudiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 28 Juni, 2022, jijini Dar es Salaam, Mhe. Nape amezitaka taasisi hizi mbili kuwajibika kwa weledi na kuwa waaminifu katika nafasi zao ili wananchi waweze kupata huduma stahiki kulingana na mahitaji yao.

“Nisisitize muwe na weledi, uaminifu na upendo vipewe kipaumbele katika nafasi zenu ili jamii ya watanzania ifaidike kwa kupata huduma bora zinazopatikana kwa wakati kila mahali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”. Alisema Mhe. Nape.

Makubaliano hayo yatawezesha kupanua wigo wa huduma za kijamii hususani katika sekta ya Afya ambapo Shirika la Posta Tanzania kupitia uzoefu wa ke katika Nyanja za usafirishaji litaweza kushirikiana na TUTUME katika usafirishaji wa bidhaa yakiwemo madawa pamoja na sampuli za damu za binadamu, wanyama na mimea kwa ajili ya vipimo kwenye maabara na mahospitalini, utafiti wa madawa pamoja na chanjo.

Aidha, Mhe. Waziri, amelipongeza Shirika la Posta kwa jitihada inayoendelea kuzifanya kwa kushirikisha wadau wa sekta mbalimbali, ikiwepo sekta binafasi ikiwa lengo ni lengo kupeleka huduma karibu zaidi na jamii ili wananchi waweze kusogezewa na kupata huduma kwa urahisi.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi ameongeza kuwa zipo fursa mbalimbali ambazo Shirika la Posta linaweza kuzitumia katika kuwafikia wananchi wengi hususani katika sekta ya usafirishaji pamoja na sekta ya utalii ambapo kupitia utengenezwaji wa Stempu zake unaweza kuhamasisha utalii ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake, Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo ameeleza kuwa Shirika la Posta nchini linaendelea kuboresha huduma zake hususani katika sekta ya usafirishaji na kueleza kuwa Shirika la Posta liko tayari kushirikiana na Taasisi na Mashirika mengine nchini

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TUTUME Bw. Misana M. Misana ameeleza kuwa kampuni hiyo iko tayari kushirikiana na Shirika la Posta nchini na kuahidi kupitia weledi na uwezo walionao kuhakikisha inafikisha huduma za kiafya kwa wananchi katika mazingira yoyote kwa kuzingatia makubaliano hayo











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...