Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wakili Msomi Dunstan D. Kyobya amesema kwamba uamuzi wa serikali kuwahamisha wafanyabiashara waliojipeleka soko la Magomeni B maarufu kama 
Soko Bati ni kuwaepusha wanafunzi na mazingira yasiyokuwa salama kutokana na mwingiliano wa watu uliosababishwa na uwepo wa soko hilo jirani kabisa na shule za Msingi Lilungu na Mivinjeni._

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema hayo wakati akiongea na wazazi wa shule ktk Viwanja vya Shule ya Msingi Mivinjeni ambapo alipata nafasi ya kusikiliza kero za wazazi pamoja na walimu na kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi kutoa kipaumbele cha miradi ya ujenzi kwa Shule hizo ili kupunguza msongomano wa wanafunzi madarasani unaotokana na uhaba wa madarasa ikilinganishwa na idadi kubwa ya wanafunzi, Shule za Lilungu na Mivinjeni ni Shule zenye idadi kubwa kuliko shule zote za Msingi Mkoani Mtwara.

 Kutokana na kero ya hamasa ndogo ya jamii ktk uchangiaji  wa huduma ya chakula,  Mkuu wa Wilaya ametoa maelekezo kwa kamati za shule kuitisha vikao vya wazazi ili kulitafutia ufumbuzi jambo hili kwa kuwa lipi ndani ya majukumu yao._

Mkuu wa Wilaya pia amewaagiza walimu wakuu wa shule za Msingi Lilungu na Mivinjeni wampelekea majina ya Wanafunzi watoro pamoja na majina ya wazazi wao ofisini haraka ili ashughulike nao kwakuwa utoro wa wanafunzi imekuwa changamoto kubwa sana ktk Wilaya ya Mtwara.

Mwisho aliwakumbusha wazazi hao pamoja na wananchi wote kujiandaa kushiriki ktk zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agost 23 Mwaka huu. Lakini pia aliwaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano ktk kuimarisha ulinzi na usalama wa maeneo yao kwa kutoa taarifa wanapoona ama kuhisi hali yoyote inayotia mashaka kwa jamii.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mtwara.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...