NA KARAMA KENYUNKO MICHUZI TV

KATIBU wa zamani wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Deus Seif, na Mtunza Hazina Abubakar Allawi, wamehukukiwa kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani na kurudisha kiasi cha sh. Milioni 13,790,000. Baada ya kupatikana na hatia katika makosa ya matumizi mabaya ya madaraka yaliyokuwa yakiwakabili.

Seif na Allawi wanakabiliwa na mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka na kujipatia zaidi ya Sh. milioni 13 kinyume cha sheria.

Mahakama imeamuru mara baada ya kumaliza kutumikia kifungo chao, Mshtakiwa Seif atapaswa kilipa fidia ya sh. 7,590,000 kwa CWT huku Alawi akitakiwa kurudisha Sh. Milioni 6.2

Hukumu hiyo iliyochukua takribani saa nane kusomwa, imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Richard Kabate.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Kabate amesema, ameridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka ambao wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa washtakiwa wametenda makosa hayo

Hata hivyo, kabla ya kuwasomea washtakiwa adhabu baada ya kutiwa hatiani, hakimu Kabate aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ndipo wakili wa serikali Imani Mitume akaeleza kuwa hawana kumbukumbu za makosa ya nyuma za washtakiwa hao.

"Mheshimiwa hatuna kumbukumbu na makosa ya nyuma ya washtakiwa, lakini kulingana na makosa waliyoyatenda na kulingana na nafasi zao kama viongozi katika chama cha walimu mbacho kinapokea michango ya walimu waliowaamini tunaomba wapewe adhabu kali

Pia ameiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mujibu wa sheria ikiwemo kurejesha fedha zote ambazo walizitumia kwa manufaa yao binafsi ili iwe fundisho kwao na kwa mwingine yeyote ambaye anaweza kutenda kosa kama hilo baada ya kudhaminiwa na chama.

Katika utetezi wake, mshtakiwa wa kwanza ameiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa anasumbuliwa na sukari pamoja na shinikizo la damu, huku mke wake pia akiwa anasumbuliwaa na maradhi ya aina hiyo. Pia amesema anaishi na mama yake ambae anamtegemea yeye na pia ana watoto wanne ambao wanamtegemea kwani bado hawajaanza kujitegemea na wote wako shuleni wanasoma.

Mshtakiwa wa pili kupitia wakili wake Nashon Nkungu aliomba mahakama impunguzie adhabu mteja wake Alawi, kwa kuwa wote ni wakosaji wa mara ya kwanza, hivyo ameiomba mahakama itoe adhabu ndogo kabisa.
"Mheshimiwa mshtakiwa ni mtu mzima anasumbuliwa na maradhi ya sukari na shinikizo la damu hivyo anahitaji kuwa kwenye mazingira mazuri . Pia anamke na watoto sita ambao wote wanamtegemea yeye.

"Nimesikiliza hoja zote na utetezi wa washtakiwa, lakini msisahau kuwa najitajidi kubaki kwenye sheria.

Pia washtakiwa wanalitumia Taifa na walishtakiwa wakiwa wanakitumia Chama cha Walimu walichoakianzisha na kukisimamia kwa nia njema," alisema.

"Kwa kuwa imesemwa wazi kuwa hawana makosa mengine, pamoja na makosa haya si kwamba hawana mazuri waliyowahi kufanya. Makosa yao yanaweza kuwa yalitokana na ukosefu wa umakini hivyo wakateleza kidogo," amesema Hakimu Kabate

"Kwa mujibu wa sheria hii mshtakiwa wa kwanza nakuhukumu kifungo cha miezi sita jela kwa makosa yote mawili, ukimaliza utatakiwa kulipa fidia ya Sh 7,590,000 kwa CWT na mshtakiwa wa pili nakuhukumu kifungo cha miezi sita jela na ukitoka utalipa fidia ya milioni 6.2 kwa CWT, " amesema Hakimu Kabate akisoma adhabu.

Kesi hiyo kwa upande wa mashtaka, uliongozwa na Wakili Imani Nitume ambaye aliwaongoza mashahidi nane mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya washtakiwa pamoja na vielelezo 12

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo kati ya Oktoba 3 hadi Novemba 6, 2018 jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kwamba washtakiwa wakiwa watumishi wa CWT, walitumia madaraka yao vibaya na kujipatia Sh. 13,930,963 kwa manufaa yao.

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa katika tarehe na eneo hilo, washtakiwa walichepusha kiasi hicho cha fedha mali ya CWT kwa kutumia nafasi walizo nazo.Mshitakiwa Abubakar Alawi aliyekuwa Mweka hazina wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) aliyevaa kanzu na Katibu Mkuu wa zamani wa CWT, Deusi Seif, aliyevaa Koti kulia, wakiwa katika ukumbi wa wazi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa hukumu ya kesi iliyokuwa ikiwakabili ya matumizi mabaya ya madaraka. Hata hivyo washtakiwa hao wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani na kurejesha kiasi cha sh. Milioni 13 kwa CWT kama fidia pindi tu wakimaliza kutumikia adhabu yao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...