Afisa Udhibiti Ubora wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Schola Mbalila akitoa mada ya udongo kwa wafanyabiashara 41 wa mbolea walioshiriki mafunzo yanayofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo ofisi ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Juni, 2022.
Afisa Udhibiti Ubora wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Schola Mbalila (kushoto) na Gema Nganyagwa kulia) wakiendelea na mada kwa wafanyabiashara 41 wa mbolea walioshiriki mafunzo yanayofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo ofisi ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Juni, 2022.
Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Happiness Mbelle akizungumza jambo na wafanyabiashara wa mbolea alipokuwa akifungua mafunzo ya biashara ya mbolea yanayofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo ofisi ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Juni, 2022
Afisa Udhibiti Ubora wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Gema Nganyagwa akieleza jambo alipokuwa akitoa mafunzo kwa wafanyabiashara 41 wa mbolea walioshiriki mafunzo yanayofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo ofisi ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Juni, 2022.


WAFANYABIASHARA wa mbolea nchini wametakiwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zinazosimamia tasnia ya mbolea na kuelezwa biashara hiyo hufanyika kwa mujibu wa sheria ya mbolea namba 9 ya mwaka 2009.

Hayo yamebainishwa leo June 28, 2022 na Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Happiness Mbelle alipokuwa akifungua mafunzo kwa wafanyabiashara 41 wa mbolea yanayofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Kilimo ofisi ndogo ya wizara Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mbelle ameeleza kuwa biashara ya mbolea inamtaka mfanyabiashara wa mbolea kupata mafunzo na kutunukiwa cheti kitakachowekwa dukani kwake ili kurahisisha mchakato wa udhibiti unaofanywa na mamlaka.

“Mkifanya biashara ya mbolea mzingatie sheria, kanuni na taratibu za kujihusisha na biashara ili kuepuka changamoto za kufutiwa leseni na kufungiwa maduka yenu.

Aidha, Mbelle amewapongeza washiriki wa mafunzo hayo kushiriki kikamilifu na kutosita kuuliza jambo lolote litakalohitaji ufafanuzi kutoka kwa wataalamu wa mamlaka.

"Muwe huru kuuliza ili mpate uelewa wa kutosha katika kujihusisha na biashara hii ili kuifanya kwa weledi na ufanisi” alisisitiza Mbelle.

Akitoa mafunzo kwa wafanyabiashara hao, Afisa Udhibiti Ubora kutoka TFRA Gema Nganyagwa, amewashauri wamiliki wa maduka na maghala ya mbolea kuwawezesha watendaji katika vituo vyao ili wapate elimu ya mbolea ambapo baada ya mafunzo watatunukiwa vyeti vitakavyopaswa kuwekwa kwenye maduka yao kuonesha uhalali wa kuuza bidhaa hiyo.

“Tusifanye maisha marahisi kwa kukwepa sheria, tusiwe wabinafsi tuwalete wanaotufanyia kazi waweze kushiriki kwenye mafunzo ili waweze kufanya kazi kwa weledi” alisisitiza N.ganyagwa

Kama taasisi tunatamani wafanyabiashara mpate mafunzo ili tunapopita kukagua na kuamua kuchukua sheria isiwe kama mnaonewa na ndio maana tunaandaa mafunzo haya mara kwa mara kuondoa visingizio.

Kwa upande wake mmoja wa wafanyabiashara Isabela Mwatebela kutoka ameiomba Mamlaka kuwasaidia namna ya kuwapata wauzaji wenye taaluma ya masuala ya mbolea kutokana na changamoto ya wauzaji hao kutotumika muda mrefu sehemu moja.

Akijibu ombi hilo Afisa Udhibiti Ubora Schola Mbalila na mtoa mada kwenye mafunzo hayo amesema taasisi inawasaidia wafanyabiashara hao kwa kuratibu na kutoa mafunzo mara kwa mara na kuwasisitiza kuwawezesha wauzaji wa mbolea kushiriki kwenye mafunzo hayo yanayotolewa bila gharama yeyote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...