*Atoa maelekezo kwa Halmashauri kuhusu utozaji ushuru tani moja ya mazao

Na Said Mwishehe, Michuzi TV -Katavi

CHAMA Cha Mapinduzi ( CCM) kimesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kukusanya mapato mengi na kuyatumia kwa faida ya wananchi kwa kujenga miradi ya maendeleo.

Akizungumza leo Julai 25,2022 na wananchi wa Kata ya Itenka wilayani Nsimbo mkoani Katavi baada ya kuweka jiwe la msingi katika Kituo Cha afya Itenka ,Kinana ameelezea hatua mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuleta maendeleo ya Wananchi huku akieleza kuwepo mengi kumechochea maendeleo.

"Serikali imeendelea kukusanya mapato na kutumia mapato kwa faida ya wananchi, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Serikali imepanga mipango yake ya maendeleo na hadi leo hapa Nsimbo kuna miradi mingi kama ilivyoorodheshwa ,kila eneo limeguswa ujenzi wa barabara kuu, barabara za vijijini na zahanati, hospitali ujenzi unaendelea.

"Kuna hospital ya Rufaa kupitia Mkoa tayari inajengwa ,umeme unasambazwa, Mkoa mzima umeme umebakia vijiji saba na mwaka huu hivyo vijiji Saba navyo vitapata umeme,nimeambiwa kuna tatizo la umeme ambao unakatikakatika na unakatika kwasababu unatumia jenereta.Sasa kazi imeanza ya kutengeneza utaratibu ili umeme unaokuja uwe wa grid ya Taifa, umeme utoke Tabora na kuja moja kwa moja mpaka Katavi,"amesema Kinana.

Ameongeza kuwa mwaka ujao wakati kama huu mradi huo wa umeme utakuwa umekamilika kwani Katavi itakuwa imejiunga na gridi ya Taifa, hivyo umeme hautakatika tena. "Naomba muwe wavumilivu na mvumilivu hula mbivu baada ya muda mfupi tutachukua haya majenereta na kuyapeleka kwenye maeneo mengine kabisa" .

Aidha Kinana amesema katika Mkoa wa Katavi kuna barabara za lami zinaendelea kutengeneza kwa kuunganisha Mkoa huo na mingine na anahakika mpaka mwaka ujao barabara hizo zitakuwa zimekamilika.

Kinana amewapongeza pia Wananchi wa Itenka na hasa Nsimbo kwa juhudi wanazofanya za kujitegemea na wamekuwa wakulima wazuri wa mpunga."Mnafanya kazi kubwa ya kuzalisha mpunga na sasa hivi naambiwa bei yake imekwenda juu ,Kuna mtu anawapangia bei?Anayepanga bei ni nani? Ni anayetoa jasho akalima

"Lakini kuuna jambo lingine nataka niseme hapa ndugu Mkurugenzi kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri unayofanya na watendaji wenzako chini ya uongozi wa Mkuu wa Wilaya kwani mnafanya kazi nzuri, hamuonekani,mnafanya kazi nzuri,hamsimami kwenye majukwaa ,hamsifiwi, mara nyingi mnalaumiwa sasa mimi nataka niwasifu kwa kazi nzuri mnayofanyaga.

"Ila kuna taratibu ,mkulima hatakiwi kutozwa ushuru wakati anaisafirisha lakini kuna malalamiko ya baadhi ya wakulima wanalalamika kutozwa ushauri.Mkurugenzi nadhani tulikubaliana kuna watu sheria wameziacha ,wanatengeneza sheria zao ,ukiwa na tani moja hakuna kusimamishwa kwani Kwa mujibu wa sheria tani moja haitozwi ushuru,"amesema Kinana.

Amefafanua isije kukawa na kuna watu wanakwenda kusimamisha wakulima wanajifanya wao ndio Serikali."Anasikmamishwa mkulima anaambiwa simama, toa ushuru,unamwambi nina tani moja unamwambia hapana,ukiuliza kwanini kwasababu ananguvu ya Serikali.Hiyo Serikali ni ya nani ? Si ya wananchi? Kwa hiyo wenye kauli ni wananchi.

"Sasa nataka niseme hivi tuelewane watakaondoa umasikini wa wananchi ni wananchi wenyewe kazi ya Serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya watu kuondokana na umasikini, tusiwasumbue wananchi,tusiwawekee vikwazo ,tusiwawekee vigingi vingi ,tusiwatoze ushuru mwiingi, kila hatua ushuru,kila hatua ushuru ndio maana muuliza karanga anazunguka kwasababu hana kituo huwezi kumtosha ushuru".

Kinana amesisitiza Serikali inapozungumza habari ya sekta binafsi,basi sekta binafsi wa kwanza ni mwananchi wa kawaida anayetafuta maisha yake kwa kulima,kwa kufanya biashara ndogo ndogo ,kuuza mifugo,duka,nyama na kwamba Mwananchi huyu anachotaka asisumbuliwe na Serikali.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrhaman Kinana akizungumza na wananchi na wana CCM wa jimbo la Nsimbo mkoani Katavi baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha afya Itenka leo Julai 25,2022 .




Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana (wa tatu kulia) akiwa ameongozana na baadhi ya Viongozi waandamizi wa chama cha CCM na Serikali mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Inteka,katika wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi leo Julai 25,2022.PICHA NA MICHUZI JR-KATAVI

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana akipewa maelezo mafupi kuhusu mradi ujenzi wa kituo cha afya Inteka mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo hicho leo Julai 25,2022.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanal mstaafu Abdulrahman Kinana akisalimiliana na baadhi ya wauguzi wa kituo cha afya Itenka wilayani Nsimbo mkoani Katavi .

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahaman Kinana akisalimiana na wanaCCM na wananchi wa jimbo la Nsimbo mkoani Katavi baada ya kufika kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha Afya Itenka,kulia  ni mbunge wa jimbo la Nsimbo Anna Lupembe.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kuhusu mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Inteka kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika kituo hicho leo Julai 25,2022.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kombe mwanafunzi wa shule ya msingi Lukama wilayani Nsimbo mkoani Katavi baada ya shule hiyo kuibuka kinara katika ya mashindano ya Pembe Cup yaliyoandaliwa na mbunge wa jimbo hilo Anna Lupembe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...