Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi Kolandoto Manispaa ya Shinyanga yamefanyika leo Ijumaa Julai 29,2022 ambapo Jumla ya wanafunzi 255 wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’.

Mgeni rasmi katikaMahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kinachomilikiwa na Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) alikuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Masumbuko amekipongeza Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kwa kutoa Programu mbalimbali na kuanza mchakato wa kuanzisha Chuo Kikuu cha Kolandoto akisema ni mipango ya mkoa wa Shinyanga kuanzisha vyuo mbalimbali mkoani humo ili kuongeza fursa za kiuchumi.

“Serikali ya mkoa wa Shinyanga inaendelea kuvutia wawekezaji mbalimbali ili wawekeze katika vyuo ili kuubadilisha mkoa wa Shinyanga…Ni fursa kwenu kuchangamkia fursa ya elimu ya juu sisi mkoa tumejipanga kufanikisha haya”,amesema.

“Serikali imeridhia kutoa sehemu ya eneo la shule ya Msingi Kolandoto ili kuongeza eneo la chuo cha Kolandoto",amesema Masumbuko.

Aidha amewataka wahitimu hao kwenda kuzingatia maadili pindi watakapoanza kuhudumia wananchi katika jamii.

“Elimu hii mliyopata ni elimu kubwa na sasa mnaenda kuingia katika ulimwengu wa kiutendaji, mnapaswa kwenda kuwa chachu, mkawe waadilifu mnapohudumia wananchi, mavazi yenu yakawe mazuri, lugha nzuri, na mkajiendeleze kielimu pia, elimu za juu zitawapa fursa zaidi za ajira”,amesema Masumbuko.

Akisoma taarifa ya chuo hicho, Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Dkt. Paschal Shiluka amesema jumla ya wahitimu wa kozi mbalimbali mwaka huu ni 255 kati yao 139 ni wa jinsia ya kike akibainisha kuwa lengo la chuo ni kuwa na 50% kwa 50% na wamevuka lengo la serikali kwa kuwa na wanafunzi wa jinsia ya kike zaidi ya 50%.

Amesema Wanafunzi 255 wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga ‘Nursingi and Midwifery’, Maabara ya Binadamu ‘Medical Laboratory Sciences’, Utabibu ‘ Clinical Medicine’, Ufamasia ‘Pharmaceutical Sciences’, na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’ ambazo zinaotolewa na Chuo cha Sayansi za Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).

“Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kilianzishwa mwaka 1957 kikiwa na Programu moja na sasa kimekuwa na ongezeko la Programu na wanafunzi kila mwaka, wahitimu wa kwanza walikuwa sita tu tofauti na tunaposherehekea mahafali haya ya 10 tukiwa na wahitimu 255”,amesema Dkt. Shiluka.

“Upekee wa mahafali ya mwaka huu, kwanza mahafali haya yameanza kwa kuwa na wiki la Mahafali ambapo kwa kushirikiana na Shirika la Doctors with Africa tumeweza kutoa huduma za afya kwa jamii na wanachuo, jumla ya wananchi 75 wamepatiwa chanjo ya Uviko 19, 100 wamepima magonjwa yasiyoambukiza, hali kadhalika kumwe na michezo mbalimbali iliyoshirikisha wanafunzi,wataaluma na wafanyakazi wa Chuo na Hospitali”,ameeeleza.

Amewataka wahitimu hao kuondokana na imani potofu ya kusubiri ajira kutoka serikalini kwani ujuzi waliopata chuoni unawezesha wao kujiajiri na kuajiri wengine.

“Mawazo ya kusubiri ajira serikalini ni mawazo potofu. Changamoto zilizopo katika jamii mzitumie kama fursa ya kujiajiri na kuajiri wengine, utaalamu mliopata chuoni utumieni kujiajiri na kuajiri wengine, nendeni mkaanzishe maabara zenu, famasi zenu na taasisi zingine kwa kadri Mungu atakavyowajalia”,ameongeza Dkt. Shiluka.

“Tunaendelea na utekelezaji wa Mpango mkakati wa miaka mitano ukiwa na malengo ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Kolandoto (-Kolandoto University - KOU) ifikapo mwaka 2026,kubaini, kupima ardhi na kuweka uzio katika maeneo yote ya chuo, kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza katika miundo mbinu wezeshi kwenye uanzishwaji wa Chuo Kikuu, kuwa na mpango rasmi (Land Master Plan) wa ardhi na kuwa na wanachuo zaidi ya 3000”,amesema Dkt. Shiluka.

Ameongeza kuwa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto kimekuwa na mafanikio mengi ikiwemo kupanua na kukarabati maabara ya kufundishia na kuweza kutumiwa na wanafunzi 100 kwa wakati mmoja, kujenga kumbi mbili za madarasa, kupanua maktaba ya chuo,kuongeza kozi ya utabibu katika Kampasi ya Mwanza, kukarabati nyumba 2 za watumishi,kukarabati hosteli 2,kuboresha maslahi na motisha kwa watumishi,kujenga vimbweta, kushiriki Maonesho ya kitaifa ya vyuo vya kati na vyuo vikuu Dodoma na kupeleka watumishi wake kwenye hifadhi ya taifa ya Ruaha.

Aidha ameomba eneo la Kolandoto liwe na kituo cha polisi na kuhamasisha uwekezaji wa nyumba za makazi eneo la chuo kwa kujenga Hosteli za wanafunzi na kuongeza huduma za kijamii.

Naye Askofu Mkuu Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota amewataka wahitimu hao watakapokwenda kuanza kufanya kazi wazingatie maadili ya kazi yao huku akiwashauri kutumia elimu waliyopata kusaidia jamii.

Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Ijumaa Julai 29,2022. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiandamana kutoka Jengo la Utawala la chuo hicho kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kwenye Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Dkt. Paschal Shiluka akizungumza kwenye Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga

Askofu Mkuu Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota akizungumza kwenye Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa Idara ya Afya wa Kanisa la AICT Dkt. Leopord Gilala akizungumza kwenye Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Mch. Juma Kiyumbi akizungumza kwenye Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Wahitimu wa Programu ya Ukunga na Uuguzi wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga

Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiwa kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga

Wazazi na wageni wakiwa kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga

Wazazi wakiwa kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
AICT Tumaini Choir ikitoa burudani kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga

Mhitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto akitoa burudani kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko  akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto. Wahitimu hao wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko  akiwatunuku Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mahafali yanaendelea.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko  akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto. Wahitimu hao wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko  akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto. Wahitimu hao wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko  akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto. Wahitimu hao wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko  akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto. Wahitimu hao wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko  akiwatunuku vyeti wahitimu wa Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto. Wahitimu hao wametunukiwa Stashahada na Astashahada katika Programu za Uuguzi na Ukunga, Maabara ya Binadamu , Utabibu , Ufamasia na Ufundi ‘ Laboratory Assistant and Computer Application’. Mahafali ya 10 ya Chuo cha Sayansi za afya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Wahitimu wa Programu ya Uuguzi na Ukunga wakila kiapo.
Wahitimu wa Programu ya Maabara wakila kiapo.
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi.
Wahitimu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi

 Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...