Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, atoa wito kwa wananchi kuendelea huduma za Shirika la Posta kwani kwa sasa Shirika limeboresha huduma zake kuwa za kisasa kulingana na mahitaji ya wananchi

Hayo ameyasema leo Tarehe 06 Julai, 2022 wakati alipohudhuria Siku maalum ya Shirika la Posta katika viwanja vya Maonesho ya 46 Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam

Aidha, Mhe. Waziri ametumia nafasi hiyo kulipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa juhudi inayoendelea kuzifanya katika kutoa huduma bora na stahiki kulingana na mahitaji ya wananchi hususani katika kipindi hiki cha maendelea ya TEHAMA

Sambamba na hilo, Mhe. Nape amepata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali viwanjani hapo ikiwemo Banda la Shirika la Posta Tanzania na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa katika viwanja hivyo

Naye, Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo ameelezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika hilo viwanjani hapo ikiwemo huduma za EMS, Duka Mtandao, Posta Kiganjani, Huduma za kubadilisha fedha za kigeni na Uwakala ikiwemo ukataji wa tiketi za ndege ya ATCL

Pia, Postamasta Mkuu ametumia nafasi hiyo kuendelea kuwakaribisha wananchi katika banda la Posta lililopo viwanjani hapo ili kuendelea kufurahia huduma za kisasa

Hafla hiyo ya Siku maalum ya Posta imehudhuriwa Viongozi waandamizi na wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania pamoja na wasanii mbalimbali wa maigizo (Bongo Movie) ikiwemo Swebe, Snura, Tausi Mdegela, Dr Kumbuka, Asha Boko, na wengine mbalimbali.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa hafla ya Siku ya Posta iliyofanyika katika ukumbi wa DOME kwenye viwanja vya Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akiteta jambo na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo wakati wa hafla ya Siku ya Posta iliyofanyika katika ukumbi wa DOME kwenye viwanja vya Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo ya huduma zinazotolewa na Shirika la Posta wakati alipotembelea banda la Posta katika viwanja vya Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akiwasili katika hafla ya Siku ya Posta iliyofanyika katika ukumbi wa DOME kwenye viwanja vya Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam. Kulia ni Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo (wa pili kulia) akiwa na Mkurugenzi Mkuu TANTRADE Bi. Latifa Khamis (kulia) Mkurugenzi mkuu wa TTCL Mhandisi Peter Ulanga (kushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa UCSAF Bi. Justina Mashiba (wa pili kushoto) wakisubiri kumpokea Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati wa hafla ya Siku ya Posta iliyofanyika katika viwanja vya Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu TANTRADE Bi. Latifa Khamis (aliyesimama) akitoa maelezo ya ratiba ya hafla ya Siku ya Posta kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (kulia) baada ya kuwasili katika viwanja vya Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Mhandisi Peter Ulanga wakati alipowasili katika viwanja vya Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...