KATIBU
Tawala Mkoani Pwani (RAS) Mhandisi Mwanasha Tumbo , amewaagiza waratibu
na wasimamizi wa fedha za Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) ,kupitia
mpango wa kunusuru kaya maskini kusimamia na kuhakikisha wanakuwa
waadilifu na waaminifu kwa fedha zinazotolewa kwa ajili ya wanufaika .
Ameeleza
yapo malalamiko kwa wanufaika Kuwa wakati mwingine fedha hizo
haziwafikii Jambo ambalo linachafua mpango mzima wa utekelezaji.
Akifungua
kikao kazi cha kujadili shughuli ya mpango kazi wa kunusuru kaya
maskini 2021/2022 ,kilichowahusisha wakuu wa idara na vitengo
sekretariet ya mkoa na waratibu wa TASAF wa Halmashauri Tisa za mkoa wa
Pwani ,Katibu Tawala mkoa huo, Mwanasha Tumbo alisema , malalamiko hayo
yanajitokeza kutokana na kuwaachia watendaji na wenyeviti wa vijiji
fedha ambapo zinachelewa kuwafikia walengwa.
Alieleza
,jumla ya kaya maskini 29,683 zinanufaika kupitia mpango wa kunusuru
kaya maskini Mkoani hapo ambapo sh.Bilioni 5.609,6 zimeshapokelewa kwa
mwaka wa fedha 2021/2022 hivyo Lazima zisimamiwe ili kutimiza azma ya
Serikali na kujiepusha na migongano.
"Pia
Utaratibu wa Sasa mnawatumia fedha kwenye simu ,mitandaoni changamoto
iliyopo walengwa wengine hawajui matumizi ya mitandao ya simu
,anamuagiza mjukuu wake ,jirani ama jamaa hadi fedha ikitoka unakuta
mlengwa anapata pungufu ama wananufaika ambao hawastahili".
Kutokana
na changamoto hiyo ,Mwanasha ameelekeza waangalie namna ya kutoa elimu
ya Utaratibu huo ili Hali wahusika wapate Uelewa.
"Fedha
hizi tuhakikishe zinawafikia walengwa na kutimiza adhma ya Serikali
kusaidia kaya maskini, Mimi mwenyewe Ni shuhuda ,nilifika pale
Kimaramisale ,Ni kati ya vijiji vipya vilivyoongezwa ,tumefika pale watu
wamepokea fedha zao na wameishukuru Serikali kwani haijawahi
kutokea"alifafanua Mwanasha.
Akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji mkoa , mratibu wa TASAF Mkoani Pwani Roselyn
Kimaro alieleza ,kaya maskini 29,683 zinanufaika na mfuko wa Maendeleo
ya Jamii (TASAF ) kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini ambapo Jumla
ya sh.Bilioni 5.609,6 zimepokelewa kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Vilevile alifafanua,ipo miradi 168 iliyoibuliwa na wananchi na inaendelea vizuri, yenye thamani ya Bilioni 1.084.
Rosely
wamepokea maagizo ya Katibu Tawala mkoa ,na watahakikisha wanasimamia
fedha hizo kwa kuimarisha ukaguzi ,na amedai wanaweka mikakati ya
kuboresha usimamizi katika miradi .
Kaimu
mratibu wa TASAF Chalinze, Sostenes Kamguna alibainisha kwamba, vijiji
52 vipo katika mpango huo kiasi cha sh.milioni 947.1 zimetolewa kwa kaya
6,011 huku kaya 3,998 wamepokea kwa njia ya simu .
Kamguna alieleza, milioni 272.190 zimeshatolewa kwa walengwa 563 kati ya 2,517 waliokidhi vigezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...