Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Shaka Hamdu Shaka ametembelea Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam.

Akiwa kwenye Maonesho hayo leo Julai 6,2022 Shaka ametembelea mabanda mbalimbali na kupata fursa ya kuona bidhaa pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na Watanzania katika sekta mbalimbali za biashara,uwekezaji, kiuchumi na kijamii.

Shaka aliingia viwanja vya Sabasaba Sasa nne asubuhi na kisha akaanzia Banda la Watoa Huduma za Bima ambapo akiwa humo amekutana na wadau wa sekta ya bima na kuzungumza nao kwa nyakati tofauti tofauti na baadae akaenda Banda la Shirika la Posta, Banda la Shirika la Reli Tanzania( TRC) na kisha kutembelea mabamba mengine na akamalizia matembezi yake kwa kutembelea Banda la wasanii.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda hayo Shaka amesema amefurahiswa na jitihada ambazo zinafanywa na Wananchi katika kuhakikisha wanashiriki katika katika kuleta maendeleo ya Taifa letu.

Pamoja na hayo Shaka amesema CCM inaridhishwa na kasi ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuondoa minyororo iliyokuwa ikidumaza sekta ya biashara na uwekezaji na kufungua milango ya mzunguko wa fedha nchini.

Amesema hatua ya Rais Samia kuondoa minyororo iliyodumaza sekta ya biashara na uwekezaji imechangia sekta hizo kufunguka na mzunguko wa fedha kuonekana."Chama chetu ya Mapinduzi kinatambua dhamira ya Rais Samia ya kuwa na mfumo shirikishi wa uongozi katika sekta zote zinazochochea uchumi."

Amefafanua kwamba mfumo shirikishi katika sekta ya biashara na uwekezaji ni muhimu katika kuleta ufanisi na kwamba Rais Samia na Serikali anayoiongoza imekuwa karibu na wafanyabiashara kwa kusikiliza changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi.Pia amefungua milango na kuondoa minyororo ambayo imekuwa ikidumaza sekta hizo.

Akielezea zaidi Shaka amesema katika Uongozi wa Rais Samia kuna mabadiliko makubwa hasa katika mzunguko wa fedha kwani umekuwa mkubwa ukilinganisha na huko nyuma na kwamba CCM imekuwa ikipokea maoni kutoka kwa wananchi wa kawaida ,wa kati na wakubwa.

Amefafanua kila wanapoongea na Wananchi wakiwemo Wafanyabishara wanaeleza wazi kuwa hivi sasa kuna mabadiliko,fedha inaonekana na inafika kwa watu."Nimpongeze Rais Samia kwa kutekeleza vema Ibara ya 49 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

"Inayoeleza katika kipindi cha miaka mitano kutambua biashara ni sekta muhimu, Chama kimeelekeza serikali kuimarisha mifumo ya biashara ili kuongeza pato la taifa na imewezekana,"amesema Shaka na kuongeza hatua hiyo erikali imefanya vizuri na kwa mwaka huu wa fedha mapato yameongezeka na kufikia sh.trilioni 22.23.

Shaka amesema hatua hiyo inajidhihirisha hata katika Maonyesho hayo na kwamba Chama chake kimeridhishwa na maandalizi na ushiriki kwenye maeneo yote mtambuka hasa sekta zinazochochea maendeleo ya biashara na uwekezaji.

"Nimetembea katika Viwanja vya Sabasaba nimeshuhudia mabadiliko makubwa ya maonyesho ya mwaka huu na ukilinganisha na yaliyopita.Mwaka huu muamko ni mkubwa na matokeo ya maonyesho hayo hayakuja kwa bahati mbaya.

"Ila kuna jitihada zimefanywa na Rais Samia," amesema Shaka na kuongeza Rais ameitangaza nchi huko duniani na kuwa kivutio katika sekta ya biashara na uwekezaji.Alihitimisha kutembelea Maonesho hayo saa tisa alasiri.





 
 
Mkurugenzi Mkuu TANTRADE Bi. Latifa Khamis (aliyesimama) akieleza jambo kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Shaka Hamdu Shaka  baada ya kuwasili katika viwanja vya Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...