Njombe


Mahakama ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imewahukumu wahamiaji haramu 37 kifungo cha mwaka mmoja gerezani au kulipa faini ya shilingi laki 5 kila mmoja kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

 

Washtakiwa hao raia wa Ethiopia wameshtakiwa baada ya kukutwa Julai 7,2022 katika kijiji cha Kidope wilayani Makete mkoani Njombe kinyume na kifungu cha 45 (1)(2) cha Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2016


Mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo Ivan Msaki, mwendesha mashitaka wa polisi Benstard Mwoshe amewasomea washitakiwa wote shitaka lao ambapo wamekubali shitaka lao la kukutwa hapa nchini kinyume cha sheria

 

Wakijitetea kabla ya hukumu hiyo kutolewa washtakiwa hao wamesema walikuwa wakisafiri kuelekea nchini Malawi na sababu ya kuondoka nchini mwao ni kutokana na maisha magumu pamoja na ndugu zao kuuawa hivyo wanaiomba mahakama hiyo iwahurumie

 

Hakimu Msaki amesema Mahakama hiyo imezingatia utetezi wao wa kuonewa huruma na mahakama hiyo hivyo akawahukumu Kifungo cha Mwaka mmoja jela ama kulipa faini ya shilingi laki 5 kila mmoja,na baada ya adhabu watatakiwa kurudi nchini mwao

 

Washtakiwa hao ni miongoni mwa wahamiaji haramu 67 kati ya 69 waliokutwa Julai 7,2022 katika kijiji cha Kidope kata ya Iniho wilayani Makete mkoani Njombe baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali na kusababisha wahamiaji haramu wawili miongoni mwao kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...