Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa wa pili kutoka kushoto akiwa msibani na waombolezaji wengine

Na John Mapepele


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan leo Julai 10, 2022 ametoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa msanii mkongwe wa Filamu nchini Chuma Seleman maarufu kama Bi. Hindu.

Salamu hizo zimetolewa kwa niaba yake na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa Magomeni jijini Dar es Salaam nyumbani kwa marehemu kabla ya kwenda kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Akimzungumzia marehemu, Mhe. Mchengerwa amesema, Mhe. Rais amemwelezea Bi. Hindu kuwa ni msanii aliyetoa mchango mkubwa katika tasnia ya Sanaa hapa nchini.

"Bi Hindu ametoa elimu ya sanaa kwa wasanii wengi sana, Serikali inatambua mchango wake. Mhe Rais amepokea msiba huu kwa msiba huu kwa mshituko mkubwa". Amefafanua Mhe, Mchengerwa

Aidha, amesema marehemu Hindu amefariki wakati Serikali inafanya mapinduzi makubwa katika sekta za Sanaa.

Katika msiba huo Katibu Mwenezi wa CCM komrade Shaka na viongozi mbalimbali wa Serikali, Michezo na Sanaa wamehudhuria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...