Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi Barabara ya Chunya-Makongorosi km (39) iliyojengwa kwa kiwango cha Lami katika sherehe zilizofanyika Matundasi Chunya Mkoani Mbeya.

………………

Na Immaculate Makilika – MAELEZO, Mbeya

Barabara ya Chunya – Makongolosi ambayo imezinduliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwa katika ziara yake ya siku nne mkoani Mbeya ni sehemu ya barabara ya Mbeya – Chunya – Makongolosi – Singida yenye kilomita 528 ambayo ikikamilika itaunganisha mikoa mitatu ya Mbeya, Tabora na Singida ambapo pia itaunganisha nchi za kusini na mashariki mwa Tanzania na kufungua fursa zaidi za kiuchumi.

Akizungumza leo, Chunya mkoani Mbeya mara baada ya kuzindua barabara hiyo kipande cha Chunya – Makongolosi Rais Samia amesema kuwa lengo la Serikali la kujenga barabara hiyo ni kuifungua Tanzania na kuongeza fursa za usafiri na usafirishaji wa bidhaa.

“Furaha yangu na faraja yangu leo ni kuona wananchi wa Matundas na Chunya kwa ujumla wananufaika na fursa ya barabara hii ambayo ikikamilika ujenzi wake kwa upande wa kusini itaiunganisha Mbeya hadi mpakani Tunduma na nchi jirani ya Zambia, mikoa ya Mbeya, Singida na Tabora pamoja na nchi za mashariki mwa Tanzania, sio tu barabara hii bali mtanufaika pia na umeme na maji masuala ambayo tunaendelea kuyafanyiakazi” Amesisitiza Rais Samia

Aidha, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa barabara hiyo ni muhimu kwa wananchi wa Mbeya kwani itasaidia kuimarisha shughuli za kilimo na biashara na hivyo kukuza uchumi wa mkoa huo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...