Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili (kulia), akimkabidhi zawadi ya kombe na vifaa vya mchezo wa Gofu mshindi wa jumla wa mashindano ya "Corporate Masters", Hussein Dewji, wakati wa fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.  Benki ya CRDB ilikuwa ni miongoni mwa wadhamini wa mashindano hayo. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Maalum, Gibson Mlaseko.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro akitupa mpira shimoni wakati wa mashindano ya mchezo wa gofu ya "Corporate Masters" ikiwa ni hatua ya fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yalifanyika kwa udhamini wa makampuni mbalimbali yaliongozwa na Benki ya CRDB.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michzo, Nape Nnauye (kulia) akibadilishana mawazo na mdau wa Mchezo wa Gofu (jina kapuni) wakati wakiwa kwenye mashindano ya "Corporate Masters" ikiwa ni hatua ya fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Katiba na Sheria Damas Ndumbaro (wa tatu kushoto), Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michzo, Nape Nnauye (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa fainali ya mashindano ya Gofu ya Corporate Masters yaliyodhaminiwa na Benki ya CRDB.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...