MKUU wa mkoa wa Mwanza Adam Malima ameiomba Tume ya ushindani(FCC) kusaidia  kudhibiti kupanda bei za vifaa vya ujenzi mkoani hapa.

Malima amesema hayo leo tarehe 18/08/2022 wakati wa semina kwa Wazalishaji ili kuwajengea uwezo katika masuala ya ushindani na udhibiti wa bidhaa bandia.

"Bei ya vifaa vya ujenzi ikiwemo Saruji, Nondo nk kwa mkoa wa Mwanza imekuwa juu hali hiyo imetokana na bidhaa hizo kusafirishwa kwa magari kutoka viwandani ambapo vingi vipo nje ya Mwanza". amesema Malima

Mkuu wa mkoa huyo pia ameiomba FCC kuchunguza na kubaini kama upandaji wa bidhaa hizo unaendana na hali halisi.

Malima amewashauri wazalishaji kulinda haki ya mlaji na  kuhakikisha wanalifikiria soko la nje ya nchi ili kukuza uchumi wa nchi na wa kwao.

Pia ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Tume hiyo katika kudhibiti tatizo la  utengenezaji na uuzaji wa bidhaa bandia.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani(FCC) William Erio, alisema tume hiyo ina lengo la kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji dhidi ya mienendo hadaifu, gandamizi na potofu katika soko.
"Tutaendelea kusimamia misingi ya ushindani ili kuweka mazingira sawa kwa wafanyabiashara katika soko." amesema

Ameahidi tume hiyo itaendelea kudhibiti bidhaa bandia  kwa kuwa bidhaa hizo zina madhara makubwa sana kwa ustawi wa wazalishaji na uchumi wa nchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani(FCC) William Erio, akizungumza na wazalishaji bidhaa kwenye semina hiyo, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Erick Mvati.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima, akizungumza kwenye semina ya wazalishaji iliyofanyika jijini Mwanza, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani(FCC) William Erio na Kaimu Mkurugenzi wa jiji hilo Erick Mvati(katikati).

Baadhi ya wazalishaji wa bidhaa wakifuatilia hotuba na mada mbalimbali kwenye semina hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...