Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya vifaa vya umeme Afrika Mashariki ya LG kwa kushirikiana na Garnet Star, imetoa ofa ya punguzo ya asilimia 33 kwa bidhaa zake kwa Watanzania, katika kipindi cha mwezi huu wa Sikukuu ya Nane Nane.

Promosheni hiyo inatarajiwa kufikia ukomo Agosti 28 mwaka huu ambapo wateja watapata fursa ya kuokoa kuanzia asilimia 10 hadi asilimia 33 ya manunuzi ya bidhaa za LG katika maduka ya Garnet Star ikiwa ni sehemu ya kusherehekea mwezi wa sikukuu ya Nane Nane nchi nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa LG kwa Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim alisema said, “Wakulima wapo kwa ajili ya kutupatia chakula sisi na taifa zima kwani kila mwaka tunasherehekea hii sikukuu ya Nane Nane.

“Tumeamua kusherekea nao katika sikukuu hii kwa kuwawekea punguzo la bei katika bidhaa zetu kwa kipindi hichi hadi Agosti 28, mwaka huu.

“Sisi kama LG, tumejiwekea mikakati ya kuendelea kuwa pamoja na wakulima na kuwaletea bidhaa mbalimbali zenye ubora zaidi ili kuendeleza ushindani sokoni,” alisema.

Alisema mteja atapata nafasi punguzo la asilimia kuanzia 10 hadi 33, lakini inategemea na bidhaa za umeme za nyumbani atakazonunua.

Vifaa mbalimbali vimeingia katika punguzo hilo vikiwemo viyoyozi, friji, vifaa vya muziki na TV.
Meneja wa Bidhaa wa LG Afrika Mashariki Eden Seo (kushoto), akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa LG Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim na Mkurugenzi Mkuu wa Opalnet Rakesh Singh, wakati wa uzinduzi wa friji mpya za LG zenye punguzo la asilimia 33 katika kipindi cha mwezi mzima wa kusherekea sikukuu ya Nane Nane jana jijini Dar es Salaam. (Na Mpigapicha Wetu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...