Meridianbet Tanzania wameendelea na utaratibu wao wa kuwa karibu na jamii, kwa kutoa sapoti kwa vijana katika shughuli zao za kuutafuta mkate wa kila siku. Tumu ya Meridianbet, wikiendi iliyopita iliwatembelea boda boda na kuwaunga mkono katika shughuli zao za utafutaji kwa kuhakikisha wanakuwa salama. Ikiwa ni muendelezo wa kugawa nyenzo za usalama wa boda boda, baada ha kutoa kofia ngumu na reflectors awamu iliyopita, wakati huu wametoa reflector nyingi zaidi kwa vituo vitano vya boda boda.
Vituo ambavyo vilitembelewa na Meridianbet ni Makumbusho, ambapo zoezi hilo lilianza likiongozwa na Twaha Mohammed kutoka ofisi ya masoko ya Meridianbet, aliyeambatana na timu ya watu watatu wengine kutoka kampuni hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...