Na. Damian Kunambi, Njombe.

Kutokana na kuwepo kwa historia ya muda mrefu juu ya kuanza kwa mradi wa liganga na mchuchuma uliopo Wilayani Ludewa mkoani Njombe, serikali imesema inakwenda kutafuta muwekezaji mwingine atakayeingia mkataba wenye tija baada ya kuhitimisha na muwekezaji aliyekuwepo ambaye ameonekana kuwa mbabaishaji.

Akizungumza hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi mkoani Njombe waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ashatu Kijaji amesema kuwa muwekezaji huyo hakuwa na nia njema kwa watanzania hivyo serikali haiko tayari kuona mradi huo unaendelea kuchelewesha.

"Mheshimiwa Rais katika miradi ile miwili ya liganga na mchuchuma kwa sasa tunaenda kuhitimisha na aliyekuwa akijiita muwekezaji kwani tumegundua siyo muwekezaji kupitia maelekezo yako Rais bali ni mdanganyifu na sasa imetosha kutudanganya", Amesema Kijaji.

Aidha kwa upande wa ulipaji fidia kwa wananchi wanaozunguka miradi hiyo waziri Kijaji amesema baada ya kukamilika kwa zoezi la sensa serikali inakwenda kuwalipa wananchi wote wanaozunguka miradi hiyo jumla ya sh. Bl. 16.

Amesema kwa tathmini ya awali iliyofanyika wananchi hao walitakiwa kulipwa Bl. 14 lakini kwakuwa ilifanyika miaka 7 iliyopita hivyo serikali imeongeza Bl. 2 na kufikia kiasi hicho cha sh. Bl. 16.

Aidha kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga ameipongeza serikali kwa hatua hiyo iliyofikiwa kwakuwa wananchi wake wamekuwa wakingoja fidia hizo kwa miaka mingi pasipo kuendeleza maeneo yao.

"Namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwakumbuka wananchi wangu, wananchi hawa walizuiliwa kuendeleza maeneo yao toka mwaka 2015 ambapo mpaka sasa ni miaka 7, kwa muda huu wote ardhi hiyo ingeweza kuwanufisha kwa kufanya maendeleo mbalimbali lakini hawakuweza kufanya hivyo kutokana na kuitii serikali", Amesema Kamonga.

Ikumbukwe kuwa mradi huu umekuwa ukisemewa bungeni mara kwa mara na mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga, huku akishirikiana na wabunge wenzie ili serikali iweze kuona umuhimu wa mradi huu.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...