Na: Mwandishi Wetu - ARUSHA

 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amepongeza Mfumo wa kuingia Mikataba ya Utendaji Kazi na Taasisi za Umma ambao unaainisha malengo yatakayo tekelezwa na Taasisi za Umma katika kipindi cha mwaka mmoja.

 

Ameyasema hayo hii leo Agosti 14, 2022 Jijini Arusha wakati wa kikao kazi cha menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu cha kufanya tathmini ya utendaji kazi wa kwa mwaka 2021/22 na kuweka malengo, na kusaini mikataba ya Utendaji Kazi kwa Mwaka 2022/23.

 

“Mfumo huu una faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuongeza uwajibikaji katika utekelezaji wa Sera, Mikakati na vipaumbele vya Taasisi za umma na vya kitaifa”

 

Pamoja na hayo Mhe. Katambi ameisisitiza menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza tija na ufanisi katika kazi tunazozifanya;

Aidha, amehimiza mshikamano na kufanya kazi kama timu kwa kuwa, Ofisi hiyo ndiyo Kioo na Kiongozi kwa Wizara nyingine, hivyo amewataka kuweka usimamizi madhubuti katika ProgramuMiradi na kazi zote ambazo zinasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu ameeleza kuwa mikataba hiyo ya utendaji kazi itasaidia ofisi hiyo na taasisi zilizopo chini yake kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kutekeleza kwa ufanisi maelekezo wanayopatiwa na Viongozi na hatimaye kuleta maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kikao kazi hicho kilishirikisha pia Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo ikiwemo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (kulia) akishuhudia utiaji saini Mikataba ya Utendaji Kazi kwa Mwaka 2022/23 wakati wa kikao kazi cha menejimenti ya ofisi hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), Jijini Arusha. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria katika ofisi hiyo Bw. Edison Makalo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akishuhudia makabidhiano ya Mikataba ya Utendaji Kazi kwa Mwaka 2022/23 kati ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria katika ofisi hiyo Bw. Edison Makalo.Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na menejimenti ya ofisi hiyo wakati wa kikao kazi cha kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa mwaka 2021/22 na kuweka malengo, na kusaini mikataba ya Utendaji Kazi kwa Mwaka 2022/23 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), Jijini Arusha. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda.



Sehemu ya menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi wakati wa kikao kazi hicho.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu akitoa mada katika kikao kazi hicho cha kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa mwaka 2021/22 na kuweka malengo, na kusaini mikataba ya Utendaji Kazi kwa Mwaka 2022/23 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (katikati aliyekaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na menejimenti ya Ofisi ya hiyo pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo. Wa nne kutoka kushoto aliyekaa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...