Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakati akifungua kongamano la siku moja la Sensa ya Watu na Makazi lililofanyika Ukumbi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida leo hii Agosti 17, 2022.



Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko akizungumza kwenye kongamano hilo wakati akimkaribisha mkuu wa mkoa ili kuzungumza na viongozi hao.

Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Singida, Naing'oya Kipuyo akitoa taarifa fupi kuhusu maandalizi ya sensa.

Kongamano likiendelea.




Kongamano likiendelea.


Taswira ya kongamano hilo.

Kongamano likiendelea.

Kongamano likiendelea. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Mesos na kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ester Chaula.

Kongamano hilo likiendelea.

Kongamano likiendelea.

Kongamano likiendelea.

Viongozi mbalimbali wakitoa heshima kwa kusimama wakati mkuu wa mkoaalipokuwa akiwasili katika ukumbi huo kuzungumza nao.

Kongamano likiendelea. Kutoka kushoto ni Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu na Mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima.

Kongamano likiendelea. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Wilaya ya Mkalama, Elizabeth Rwegasira na kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi, Winfrida Funto.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye kongamano hilo.


Kongamano likiendelea. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa na kushoto ni Mwenyeiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Eliya Digha.


Na Dotto Mwaibale, Singida



MKUU wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewakumbusha viongozi na wananchi wa mkoa huo kutumia umakini,weledi, nguvu na akili kutekeleza zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23 mwaka huu.

Serukamba alitoa kauli hiyo leo Agosti 17, 2022 wakati akifungua kongamano la siku moja la sensa ambalo limewahusisha , wabunge, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu Tawala,Makatibu Tarafa, madiwani kutoka kata zote 136, watendaji wa kata, viongozi wa CCM, viongozi wa dini na wajumbe wa kamati ya sensa ya mkoa.

"Napenda kuwakumbusha viongozi na wananchi wenzangu wa Singida kuwa katika mambo ambayo tunapaswa kuyafanya kwa uaminifu, umakini, weledi na kutumiĆ  nguvu na akili zetu zote kulitekeleza ni Sensa ya Watu na Makazi kwa sababu ndiyo itakayotuletea huduma pale zisipokuwepo, kutuongezea na kuimarisha huduma pale zilipo" alisema.

Alisema Serikali na wadau wa maendeleo hawaleti tu huduma kwa watu kwa kuwa tu ni mafundi wa kusema bali ni kwa kutumia takwimu za idadi ya watu na nyingine zitokanazo na tafiti mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya takwimu.

Serukamba alisema hana mashaka na uwezo wa viongozi hao kwani wamejidhihirisha tayari wao na umahiri wao kwa kila wakati kwa kupeana majukumu.

" Nawashukuru sana kwa ushirikiano wenu tangu zoezi la Sensa ya majaribio kwa yale maeneo yaliyohusika hadi Zoezi la Anuani za Makazi" alisema Serukamba.

Aliwata viongozi hao ambao ni wenyeji wa makarani wa Sensa katika maeneo yao waende kufanya kazi kwa weledi ili kuitumikia nchi yetu kwa ufanisi wa utendaji wa makarani wa Sensa ambao utategemea ushirikiano wao.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko alisema lengo la kongamano hilo ni kutokana na umuhimu wa viongozi hao katika zoezi hilo na kuongeza nguvu ya ziada ili kulifanikisha.

Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Singida, Naing'oya Kipuyo , alisema Mkoa wa Singida utakuwa na makalani na wasimamizi wa sensa 5,499 ambao watasimamia zoezi hilo la sensa.

Alisema umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni pamoja na kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa;

Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali.

Kipuyo alisema Mkoa wa Singida umejipanga kufanya zoezi hilo kwa weledi mkubwa na kuwa mmoja wa mikoa ambayo inatarajia kufanya vizuri baada ya wasimamizi na makarani hao kuwa tayari kuifanya kazi hiyo kama walivyoelekezwa katika mafunzo waliyopata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...