Picha ya pamoja Mgeni rasmi Naibu waziri wizara ya Habari na Mawasiliano ya teknolojia ya Habari Kundo Mathew, Mkurugenzi Mkuu wa tume ya Tehama Nkundwe Mwasaga pamoja na viongozi mbalimbali kutoka katika Mashirika na taasisi zisizo za Kiserikali wakiwa pichani mara baada ya kufungua Jukwaa na Kongamano la Kidigitali Kwa Maendeleo ya vijana wakitanzania kunufaika na fursa za Mabadiliko ya matumizi ya TEHAMA.
Vijana mbalimbali waliohudhuria Jukwaa na Kongamano la Kidigitali kwa vijana 2500 kupata fursa za kiuchumi linaloendeshwa Kwa siku 4 kuanzia septemba 16 Hadi 19 Jijini Dar es salaam

   
Na.Khadija Seif, Michuzi TV

KUKOSEKANA Kwa ajira Kwa vijana taasisi na Mashirika mbalimbali yasio yakiserikali yameamua kuwajenga uwelewa Vijana katika kujikwamua kiuchumi kupitia fursa za Kidigitali katika Mabadiliko ya matumizi ya TEHAMA.

Akizungumza wakati wa kufungua Jukwaa la Kidigitali Kwa Maendeleo ya vijana ,Naibu Waziri wa Wizara ya Habari na Mawasiliano ya teknolojia ya Habari Kundo Mathew amesema Serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi wameamua kuwajenga uwelewa Vijana Kwa namna ya kufanya fursa za Kidigitali katika Mabadiliko ya Tehama kuwa sehemu ya fursa za kibiashara na kujikwamua kiuchumi kwani Serikali haiwezi kuajiri watu wote nchini.


Hata hivyo Mathew amesema kupitia Serikali imeweka sera wezeshi itakayosaidia vijana kupata ajira kwa njia ya Mitandao ikiwemo kutengeneza matumizi au programu zitakazotumiwa katika mifumo ya kibiashara na matumizi kwa jamii .


"Kupita jukwaa la na Kongamano la vijana wa Kidigitali wapatao 2500 kutaweza kurahisisha upatikanaji wa program mbalimbali pamoja na fursa za ajira kutoka ndani na nje ya nchi hivyo tutaweza kupata wataalam wapya katika taifa letu ".


Pia ameongeza kuwa Serikali inaandaa mchakato wa kutunga sera itakayoweza wataalam wote wapya wa program mbalimbali kupewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao Ili kutambulika kwa haraka na kupata fursa Kimataifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa tume ya TEHAMA Nkundwe Mwasaga amesema tume ya TEHAMA inahakikisha inatumia Vijana kuwasaidia kujenga ueleewa katika fursa za Kidigitali pamoja na kuwakuza katika tehama.

"Sio kuwajenga tu ueleewa bali itahakikisha inafungua milango ya fursa na kuwakuza bila kujali Elimu yao ili kutengeneza wataalam ambao watakua wazuri kutangaza taifa letu katika Mabadiliko hayo mapya ya TEHAMA katika fursa za Kidigitali na kutegemea uwekezaji mpya kutokana na fursa hizo".

Meneja Mawasiliano na ushirikiano kutoka Taasisi ya fursa za Kidigitali (DOT) Ndimbumi Msongole ameeleza namna taasisi hiyo Inafanya juhudi kuhakikisha vijana wanapata fursa bila kujali wametoka maeneo yapi kuanzia mjini hadi vijijini hususani kwenye sehemu zinazopata mkongo wa taifa kwa uzuri zaidi.

Pia ameongeza kuwa Kwa Sasa takribani Mikoa 11 imekua nufaika na jukwaa la fursa za Kidigitali na Maendeleo Kwa vijana lengo ni kusaidia vijana pamoja na Serikali kuwezesha upatikanaji wa ajira kwa haraka zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...