Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Sikonge

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amewataka watumishi wa umma waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi wilayani Sikonge kwenda kutatua changamoto walizonazo.

Shaka ametoa kauli hiyo Agosti 18,2022 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Sikonge alipokwenda kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwahimiza watumishi kufika kwa wananchi.

“Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ina kilometa za mraba 27,873 , ni Wilaya kubwa, hakikisheni mnasimamia maendeleo lakini muwe mnafuatilia huduma za kijamii mpaka huko vijijini, vitongojini.

“Baadhi ya maeneeo hamfiki , Mbunge amesema ujenzi wa mabarabara ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amerahisisha usafiri na usafirishaji , niwaulize mnakwama wapi?

“Ukitoka hapa kwenda Kipili ni kilometa 400 lakini wananchi wanalalamika huduma za kijamii zimekuwa ni dhaifu ,wanapohitaji kutatuliwa matatizo yao mambo hayaendi vizuri, shida nini? Changamoto iko wapi?Alihoji Shaka.

Amewaomba watumishi na watendaji waliopewa mamlaka kwenye halmashauri kumsaidia Rais Samia kwa kuwafikia wananchi na kutatua kero zao na changamoto zao.

“Ndio jukumu tulopewa , tusipofanya hivyo itakuwa ni sehemu ya kwamishana na mambo hayataenda vizuri. Sisi kazi yetu ni kuongeza kasi na spidi ili wenzetu waliopewa dhamana serikalini wafanye vizuri zaidi,”amesema Shaka.

Aidha Shaka amezungumzia barabara inayounganisha Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora na Chunya mkoani Mbeya ambapo taarifa alizonazo tayari maandiko ya kuomba fedha yameandikwa, hivyo watakwenda kusukuma andiko hilo ili barabara ijengwe kwa kiwango cha lami.

Amesema barabara hiyo ni muhimu katika kukuza uchumi wa pande zote mbili kwani hata kiwanda cha nguo Mbeya kinategemea barabara hiyo na sasa kimefungwa.

“Moja ya kazi kubwa inayofanywa na wana Sikonge ni uzalishaji wa pamba kwa sasa hivi usafirisaji na hapa mlikuwa mnasafirisha kwa karibu zaidi ni kwenda Mbeya , taarifa nilizonazo kiwanda cha kuzalisha nguo cha mbeya kimegungwa.

“Sababu iliyosababisha kufungwa kiwanda kile ni kukosekana kwa barabara na taarifa nilizonazo andiko limeandikwa kutafuta fedha sehemu yoyote ili kuifungua barabara hi kusudi kuimarisha uchumi wa wana Sikonge lakini kuimarisha uchumi wa wana Tabora .Barabara hii inaunganisha mkoa wa Tabora na Mbeya Shinyanga itakuwa inasafirishwa kupitia barabara hii ya Ipole –Rungwa,”amesema Shaka.

Katika hatua nyingine amesema katika Kata ya Tumbi kumepita mradi wa reli ya mwendo kasi lakini changamoto kubwa iliyoko ni kutokamilika kwa tathimini ya ule mradi ili wananchi walipwe fidia .

“Kuna siku itabidi tuende huko TANESCO wanakwamisha ili fidia ya wananchi isiweze kukamilika.Niwaombe sana watu wa TANESCO hebu waharakishe ili jambo limalizike ili kusudi kasi ya mradi huu kama alivyodhamira Rais imalizike kwa wakati, “amesema Shaka.

 

Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Sikonge waliohudhuria mkutano wakati wa Ukaguzi wa maendeleo ya Upanuzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...